Msaada wa mawazo

carmel

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2009
Posts
2,836
Reaction score
265
Habari zenu wakuu,

Kuna mtu wangu wa karibu alikuja kutoka nje, anahitaji kutoa sadaka kwa ajili ya msimu huu wa easter lakini asingependa kupeleka kanisani na badala yake anapenda kupeleka kwenye vituo vya kulelea yatima, any one with ideas ya wapi kituo kipo na infor za aina hiyo? thanks
 
Vituo vya watoto yatima nadhani vipo vingi, suala ni kuwa anataka kutoa vituo vya mkoa gani?
 
mmmhhh Mungu ambariki zaidi.... yuko mkoa,wilaya gani Carmel au anaweza safiri nimwalike huku kijijini kwetu?
 
Vipo vingi sana dar..unaweza kwenda msimbazi centre kuna kituo cha watoto yatima pale..kiko chin ya masister wa roman catholic church.
 
msimbazi center........hapo ndo naendaga hata mimi.......
 
Kipo kingine Kurasini.

Ila msaidie ili awe mwangalifu na Bongo. Kwa tangazo hili usishangae kusikia Mzee DC kaanzisha kituo leo na kesho kikawa na watoto yatima wa kutosha. Bongo watu hawakawii kucheza sarakasi..ni wasanii wa nguvu kuanzia wenye magamba laini hadi wale wenye dizaini ya kobe!!
 
Safi sana MUNGU AMZIDISHIE BARAKA ZAIDI.
 
Kama walivyoeleza wana JF, ni kweli vituo viko vingi sana pia anahitaji kuwa makini ktk kutoa huo msaada. Ushauri wangu hapa ni kwamba kama inawezekana ajitahidi kutoa msaada wa vitu kulipo pesa talimu ili kupunguza uwezekano wa ubabaishaji kwa baadhi ya watu ktk baadhi ya vituo.

Mungu ambariki na kumzidishia alipotoa.
 
anataka hapa dar

msimbaz centre
kwamama theresa mburahat
jesh la wokovu
tandika maguruwe
tmk mwisho

nipm nkiwambie
bt ni vzuri ukawachek kwanza cz minaendaga pale msimbazi center kwa mwez mara mbili (jumamosi mbil za mwez hali ya pale si mbaya wana full materials
wanapata msaada toka nje
sema wafanyakaz wa pale ndo hali ao mbaya
km ukiwaWEZESHA KUWASAIDIA WALE WANAOWASAIDIA WATOTO PALE UTAKUWA UMEFANYA KITU KIKUBWA SANA
WATOTO WANAPATA NGUO NZUURI NA VYAKULA TOKA NJE


NA KWA MAMATHERESA THE SAME...KUNA VILE VTUO VYA MTAANI NI KWELI WANA SHDA AMBAO HAO NI RAHISI KUWAPATA..JUST GO TO OFISI ZA WILAYA WATAKUPA VTUO VYOTE VYA WATOTO YATIMA THEN UTACHAGUA MWENYEWE...


km wapenda naweza kukusaidia...nchek.

nb; kuna wazee wasiojiweza pale msimbaz centre km utaweza kuwainclude umo its ok..ni vlema,wagonjwa na hawana ndg....
 
Rose1980, umemaliza kilakitu. carmel fanyia kazi hii:hat:
 
tatizo la walio wengi wanapenda lkupeleka misaada vituo vyenye majina na vinavyopata misaada mikubwa kila kukicha kama dogodogo, msimbazi, mama theresa na kusahau vingine ambavyo vina hali mbaya...nashauri tu, aende vile ambavyo havina msaada sana hivi vya theresa, msimbazi awaachie wanasiasa na zawad zao za pasaka
 

Lengo hasa ni vile vituo ambavyo havina msaada kabisa, hivyo ambavyo tayari vina hali nzuri ni vema vikawa out of list. asanteni kwa mawazo yenu lakini wengi pia mmention tu sehemu bila kutoa full address au maelekezo ya kufika hapo. Rose ntakupm
 
Lengo hasa ni vile vituo ambavyo havina msaada kabisa, hivyo ambavyo tayari vina hali nzuri ni vema vikawa out of list. asanteni kwa mawazo yenu lakini wengi pia mmention tu sehemu bila kutoa full address au maelekezo ya kufika hapo. Rose ntakupm

Mwambie apeleke kituo cha Don Bosco Kimara Suka motel. Kituo kiko opposite na kituo cha daladala cha suka kuelekea town. Pale pana hali mbaya sana kama still hakijahamishwa. Be blessed,
 
Kuna kituo cha wazee Kigamboni, pia anaweza hata kwenda shule za kata kwani hizo hazina madawati na msaada wake utadumu zaidi na zaidi kwani atasaidia future generation

Na ukizingatia shule za kata hazina dini basi atafikia walengwa wa ukweli...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…