msaada wa mawazo

msaada wa mawazo

CharmingLady

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2012
Posts
18,296
Reaction score
12,972
habari za jumatatu wapendwa, hope w-end yenu ilikuwa poa kama yangu. naomba tumshauri rafiki yangu.
yeye anatarajia kuolewa katikati ya mwezi ujao. anauliza ni zawadi gani nzuri anaweza kuwapatia kaka zake (kama zawadi za marehemu wazazi wake). kama mjuavyo wakati wa send off bi.harusi mtarajiwa huwapa wazazi zawadi / shukrani. basi naye anatafuta zawadi ya kuwapatia kaka zake ambao wamemlea kama ambavyo angelelewa na wazazi wake. asanteni
 
awaandikie shairi lenye ujumbe mzito kuhusu "UMUHIMU wa matumizi ya CONDOM" ni mawazo yangu.
 
simple anaweza nunua mashati mazuri akayafunga vizuri kwenye gift papers akawapa siku hiyo.........

Au la kama ana hela awanunulie vitu ambavyo hawana, ila sioni sababu ya kucomplicate mambo.......
 
asante kwa ushauri BT
 
habari za jumatatu wapendwa, hope w-end yenu ilikuwa poa kama yangu. naomba tumshauri rafiki yangu.
yeye anatarajia kuolewa katikati ya mwezi ujao. anauliza ni zawadi gani nzuri anaweza kuwapatia kaka zake (kama zawadi za marehemu wazazi wake). kama mjuavyo wakati wa send off bi.harusi mtarajiwa huwapa wazazi zawadi / shukrani. basi naye anatafuta zawadi ya kuwapatia kaka zake ambao wamemlea kama ambavyo angelelewa na wazazi wake. asanteni
ana budget kiasi gani ? kama vp anunue linen ful shati na suruwale
 
aangalie kitu gani hao kaka hawana kuendana na mfuko wake.....anaweza nunua sandals, au mashati simple mazuri
 
anaweza nunua shati nzur na saa nzur za mkononi. ndo wazo langu
 
inategemea kama anakaa nao nyumba moja anaweza nunua pambo zuri la nyumba yao frem nzuri ya expensive ambayo its an everlasting memory kwa mmja mmja will vanish.au frem ya picha nzuri aweke picha nzuri ya kila mmja small picture(family frem )kuna mahali zinauzwa huku kisutu kwa waarabu flan yani ni nzuri sana.
 
Awaulize wakubwa zake heshima na desturi za kabila lake...
Najua zawadi za kimila huwa haziwi kubwa sana,lakini huwa zina maana sana.
Wakati mwingine huenda ikawa ni nguo, shuka, bakora, msuli n.k.
Kuna wakati niliambiwa,ukimnunulia binti wa kimaasai saa ya mkononi ni sawa kabisa na kumvisha pete ya uchumba
 
nashukuru kwa ushauri!
 
dad una busara sana kama binti yako!
 
Mimi naamini kama ameishi nao anawafahamu vizuri sana,Wakati mwingine maneno yandani yanafsi kama shukrani huwa nishukrani tosha!Then kama atakuwa nachochote anaweza toa.Akae nao once kwakuwaomba japo masaa machache kwapamoja ajimwage apricition zake kwao,naami nao watakuwa nalao tamu kwake!
 
Back
Top Bottom