Msaada wa mawazo

geu

Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
7
Reaction score
0
Ni vyema kuacha kazi ili kwenda kujitolea kwenye ofisi ambayo itakusaidia kupata kazi nzuri.
 
Ni vyema kuacha kazi ili kwenda kujitolea kwenye ofisi ambayo itakusaidia kupata kazi nzuri.

uzi wako una maelezo mafupi mno wala hujaeleweka vizuri funguka zaidi ili watu wakushauri unataka nini haswa
 
Hiyo ni bangi yaani uache kazi unayolipwa hata kidogo ukafanye bure, huko unakotaka kwenda je wamekupa uhakika wa ajira?
 
baki hapo unapolipwa hata kidogo kuna waliovolunteer mwaka kazi zikatoka hawakuwa considered. pia unaweza ukaenda kuvolunteer usipewe hata 10000. so endelea na kazi volunteer zitakuletea stress
 
ishu ni kwamba mi ni mwalimu wa sekondari nafanya kazi serikalini kwa muda wa miaka 5,niliamua kijiendeleza kwa sasa ninashahada ya maendeleo ya jamii na uchumi, nimetafuta kazi muda mrefu kwa ngazi ya shahada sijabahatika, kuna siku niliona tangazo la kuvolunteer kwenye NGO inayoitwa africa volunteer corps. niliomba nikafanya nao interview nimeitwa nikafanye nao kazi watanilipa kiasi kidogo cha fedha, chakula na malazi ni juu yao.Lengo langu ni kupata uzoefu kwenye hii kazi ya maendeleo ya jamii.
 
sio bure kabisa ndugu nitalipwa kidogo
 
Unachezea kazi wewe, tulia hapo ulipo maana ukiwa na kazi ni rahisi kupata kazi
 


Wewe utakuwa ni mwalimu wa sekondari na umeajiriwa kwenye halmashauri, kama ni hivyo kuna utaratibu wa kuomba kubadilishiwa kazi kwa kiingereza inaitwa recategorization hapo hapo kwa muajiri wako, nakushauri kama unataka kufanya kazi za maendeleo ya jamii nenda kwa afisa utumishi kaongee nae atakufafanulia vizuri inawezekana kukawa na upungufu wa watumishi kwenye idara ya maendeleo ya jamii ukawa recategorised huko.
Sikushauri uache kazi kabla ya kupata kazi nyingine
 
Reactions: EMT
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…