Msaada wa mawazo

Msaada wa mawazo

olivier

Member
Joined
Feb 8, 2013
Posts
5
Reaction score
0
Nina mtoto mchanga ila maziwa yamekata ghafla na yanayotoka ni mepesi sana mtoto hashibi,nifanyeje yaongezeke uzito na wingi
 
Kunywa sana uji wa ulezi na vyakula vyenye lishe kubwa.
 
Nina mtoto mchanga ila maziwa yamekata ghafla na yanayotoka ni mepesi sana mtoto hashibi,nifanyeje yaongezeke uzito na wingi

Pole, ni mtoto wa ngapi kujifungua? Leo ni siku ya ngapi baada ya kujifungua? Ulipata shida yeyote wakati wa kujifungua...hasa kutokwa damu nyingi?
 
Nina mtoto mchanga ila maziwa yamekata ghafla na yanayotoka ni mepesi sana mtoto hashibi,nifanyeje yaongezeke uzito na wingi

kunywa supu asubh kwenye saa moja...then kila baada ya masaa 4 kunywa mtori hpe waujua if not ulizia mchaga yeyote hapo.usijinyime kula hata kdg...binafsi nilipata tatzo kama hilo lako ila kwa sasa kichanga kinashiba kabisa.
Pia kuna chakula kinaitwa kitawa/kena ni cha kichaga pia.ndizi zinapikwa zen zinapondwa na kuwa lain kisha unaweka maziwa mgando..ni aina ya mtori ila hapa ndizi zinazotumika ni ngumu na badala ya kuweka nyama unaweka maziwa mgando.
 
Kunywa sana uji wa ulezi na vyakula vyenye lishe kubwa.

uji wa ulezi huwa unaleta constipation...kama umejifungua kwa c-section itakuletea shida labda usubiri till after 2month.
 
Ni mtoto wa pili ana miezi 2,labour ilikua ngumu na masaa mengi,na yes damu nayo ilikua nyingi
 
Kula lishe mzito mama, na kwa chakula kingi na tia pilipili maziwa yatatoka tu.
Kula ugali na samaki, nyama, mboga za majani, maarage, nk
viazi, mihogo, ndizi, mseto, lishe mzito.

kwani unakula chakula gani mwenzetu

Ukishinda na njaa na ukinywa chai tu na chapati, maandazi, maziwa yatato toka
 
ulezi sio mzuri. kunywa mitori, supu, uji wa sembe na kunywa walau lita moja ya maziwa fresh ya moto kila siku.
 
Back
Top Bottom