msaada wa mawazo

karema

Member
Joined
Oct 3, 2013
Posts
95
Reaction score
7
nimeanzisha kampuni ya kuzoa taka,lakini nashindwa nianze vipi kazi,kama mnavyojua wabongo walivyo wagumu kutoa pesa,lengo la kampuni yangu ni kuzoa taka majumbani hapa mbeya,hembu nipeni mawazo,how should i do to get into the field,nategemea kucreate more employement.
 
Nenda serikali za mitaa ujaribu kuzungumza na Mwenyekiti kuhusu kampuni yako, alafu omba upate tenda ya kuzoa taka katika maeneo husika wao watasambaza barua katika kila nyumba ya kuwajulisha kuhusu mchango wa uzoaji wa takataka.

Ila lazima katika maongezi yako uoneshe namna serikali za mitaa zitakavyoweza kujipatia kipato kupitia mradi huo uliounzisha.

Kwamfano; unaweza kutoa pendekezo la kukusanya shilingi 4000 kila mwezi kutoka katika kila nyumba na kila fremu ya biashara inajitegemea sh.4000 pia. Alafu ukawaambia kwamba kila 4000 watajipatia shilingi 1000.

Hapo itakuwa rahisi kwa wao kukubali kwa haraka kwakua na wao watanufaika.

Cjajua kwamba una vifaa vyote vinavyohitajika au la?

Lakini kiukweli ni mradi wenye faida kubwa sana kwani kuna;

Idadi ya nyumba 250
gharama kwa nyumba x4000
Jumla Tsh.1000000.
Inamaana kwa kila mwezi unaweza kujikusanyia milioni moja za kitanzania kwa nyumba 250.

Kwa maelezo zaidi ya namna ya kuendesha biashara yako ni pm tutaelewana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…