Msaada wa mawazo

sam-Akida

Senior Member
Joined
May 20, 2013
Posts
115
Reaction score
97
Habari ndugu zangu.

Nimeshindwa la kufanya na kushauri, mdogo wangu kahitimu diploma ya ualimu ila ana mapenzi sana na IT yuko kazini tangu 2013 anahitaji kwenda kusoma ila ni kipi akasomee kaniuliza nimeshindwa kumjibu.

Je mwanishauri nini ili nimsaidie maana yaelekea hafurahii kubaki ktk ualimu.

Asanteni sana.
 
Sasa kama ana mapenzi na IT na hajui akasomee mini basi tayari hilo ni tatizo namba Moja

Kumbuka umesema yeye ni mwalimu na yuko kazini mwaka wa tatu sasa, kwahiyo huyo ni mtu mzima na anategemewa hata na jamii anamoishi kwa ushauri na miongozo mbalimbali, hivyo asimame kama yeye na kuwa na maamuzi binafsi
 
asante ila anahitaji kuongeza elimu . kiufupi bado umri mdogo, je ni fani gani itayomfaa aweze kusomea. anataka kuhama fani
 
asante ila anahitaji kuongeza elimu . kiufupi bado umri mdogo, je ni fani gani itayomfaa aweze kusomea. anataka kuhama fani

Ni vema mwenyewe akasema anataka awe nani katika maisha ni muhimu mno la sivyo atayumba sana kwakuwa anaweza afanye kitu ambacho hakiko rohoni mwake

Siku hizi watu wengi wanavurunda kwakuwa wanafanya kazi ambazo hawakuzipenda ila ama walifuata maslahi au hawakuwa na chaguo lingine

Ni ngumu kumchagulia kwasababu hata hatufahamiani na wala hatujawahi kuonana popote LAKINI kama atapenda kupokea ushauri wangu arudi darasani akajifunze vitu viwili, Lugha ya kichina na sheria
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…