msaada wa mirath

Anita Baby

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2011
Posts
1,265
Reaction score
540
endapo baba aliwahi kuoa wake wanne kwa wakati tofaut tofauti yani anaoa af anaachana nae kisha anaoa mwingine. kumbuka ktk wake hao wanne alijenga namke wa pili tu. na huyo mke ambae badozyipo nae amaish nae kwenye nyumba alojenga na mke wa pili. je ni nan mrith halal wa hiyo nyumba? watoto wote au wa yule alojenga nae?
 
Tukizungumzia mke wa kurithi ni huyo mke ambaye wakati mume anakufa yeye alikuwa bado ni mkewe ( hakuwa ameachwa) ama kwa watoto ni watoto wote wa mume bila kubagua alizaa na mke wa kwanza au mwingine
 
kunamambo mengi sana hapa....mume alikuwa dini gani? Alioa mke wa kwanza kwa sheria gan? Waliachana kwa taratbu za kimahakama, yaani talaka ilitolewa ama la? Maisha yake wakati wa kufa yalikuwaje? Ameacha wosia wowote? Walijengaje na huyo mke wa pili, nani alitoa nin.
 
Sijui sheria inasemaje lakini ninavyofahamu ni kuwa wale walioachwa kutokana statute limitation hawana haki kwani haki wangedai baada ya kutolewa talaka na kwa vile muda mwingi umepita hawana chao
Watoto wote bila kujali alizaa na mke yupi ni warithi halali wa mali za baba yao
Mke/wake ambao wakati mauti unamfika walikuwa bado mke/wake zake nao ni warithi pia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…