Msaada wa miziki, please.....

Sikonge

JF-Expert Member
Joined
Jan 19, 2008
Posts
11,584
Reaction score
6,136
Wana JF,
Kukaa shamba nako kuna shida zake.

Kuna miziki naitafuta sana. Nimevuta kwenye YOUTUBE ila quality yake mhhh. Ninaomba kama kuna mtu ana MP3 ya quality nzuri hasa ningelipenda kuanzia 192kbps, ingelikuwa mswano sana. Nyimbo kwa leo naomba mbili tu.
1.PAPITHO LAS ( Manda Chante )

[ame]http://www.youtube.com/watch?v=LtirsYpC1kw[/ame]

Huu wa pili naomba kama mtu anafahamu wimbo waitwaje na mwimbaji alikuwa nani kama mtu hauna basi waweza nisaidia jina kama wafahamu. Tatizo huyo aliyeweka wimbo sijui kama alipatia. Nimejaribu kuutafuta kwa jina hilo kwenye google nimekwama. Please please fanyeni msaada.

2. Midnight Express feat. Yvonne Chaka Chaka - Everyday Everynight.

[ame]http://www.youtube.com/watch?v=r5XqEzdqcMI&feature=related[/ame]
 
Miziki si neno la kiswahili, wingi wa muziki/ mziki ni muziki/mziki.

Unaweza kusema wimbo/ nyimbo ukitaka kuweka wingi, lakini si muziki/miziki.
 
Miziki si neno la kiswahili, wingi wa muziki/ mziki ni muziki/mziki.

Unaweza kusema wimbo/ nyimbo ukitaka kuweka wingi, lakini si muziki/miziki.

Ebwana una uhakika "miziki" sio neno la Kiswahili?
 
Miziki si neno la kiswahili, wingi wa muziki/ mziki ni muziki/mziki.

Unaweza kusema wimbo/ nyimbo ukitaka kuweka wingi, lakini si muziki/miziki.

Bluray,
Vyovyote vile itakavyokuwa. Mie shida yangu ni hiyo miziki au nyimbo kama unavyosema. Hivyo ngoja niandike:

Jamani mwenye NYIMBO hizo mbili hapo juu, namuomba.
 
Ndiyo kwanza nimeipata DVD + CD ya Manda Chante ya Delivrance Totale. Doo, ni tofauti sana na hiyo Video ya Youtube maana quality hadi unakataa kuondoka. Nashukuru kwa wote waliosoma na kwa njia moja au nyingine wakata kusaidia.

Ila ule wimbo wa pili bado sijaupata (Midnight Express feat. Yvonne Chaka Chaka - Everyday Everynight.) Kama mtu ataubahatisha sehemu basi tujulishane. Hata kama unafahamu sehemu unauzwa basi nijulishe tuwasiliane juu ya malipo na usafiri. Thanks again.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…