Msaada wa namna ya kuhamisha nguzo ya TANESCO

Hata kwangu chanika mmenifanyia haya tena toka nguzo inawekwa nawaambia hapa mnaweka juu ya kiwanja changu wale mafundi wananijibu "huwezi kutuzuia" kwahiyo nguzo imewekwa makusudi halafu baadae niingie gharama kuhiamisha kweli?
Wateja huwa wanashirikishwa kuonyesha eneo ambalo umeme unapaswa kupitishiwa aidha kwa ambao nyaya zitapita juu ya viwanja vyao huwa wanapaswa kukubaliana na majirani zao kwa maandishi.Tulitarajia kama hilo limetoka bila ridha yako ungetoa taarifa mapema
 
Mkuu hapa kwangu nahisi kuna mazingira ya rushwa, waliokuwa wanapelekewa umeme walimuhonga mwenyekiti wa mtaa, binafsi nimetoa eneo langu litumike kama barabara so nilitegemea tanesco wangepitisha nguzo pembezoni mwa hiyo barabara cha ajabu wamepitisha katikati ya eneo, pili hawa tanesco mbona wameshindwa kutumia hata weledi kidogo? Yaani wao ni kupitisha tu wanapojisikia?
 
Usiwe na shaka tafadhali fika ofisini wataalamu wetu watakuja hapo na mgogoro utamalizika kwa kuwa sasa tunasikikiza upande mmoja wakati tunapaswa kusikiliza wote
 
Usiwe na shaka tafadhali fika ofisini wataalamu wetu watakuja hapo na mgogoro utamalizika kwa kuwa sasa tunasikikiza upande mmoja wakati tunapaswa kusikiliza wote
Sawa mkuu
 
Wakiwafanyia makusudi we usiumize kichwa tafuta asid mwagia nguzo itakuja anguka yenyewe tu ... Hii bangi navutaga nitaiacha tu
 
Gharama za nini ninyi ndo mmepita kwenye kiwanja cha watu?
 
He!! Gharama ni kwa mwenye eneo au mteja wenu?
Hapo hata mm nashangaa, kawaida kabla haujapitishwa umeme lazima lizaa ya mwenye eneo husika iwepo, na sio katikati ya kiwanja Saveya wa Tanesco alichemsha.
 
Hii gharama ni kwa aliyeomba nguzo ihamishwe kutoka eneo lake kwa kuwa hawezi kuomba mwingine nje ya eneo husika.
Asante nina tatizo linaofanana sawa na la mleta mada nashukuru kwa maelezo yako kwenye uzi huu.
 
Hayo yatabainika mara baada ya wataalamu wetu kufika eneo lako
Hapa ninapoishi nilikuta tayari nguzo ya umeme ipo katikati ya barabara, kati yangu na jirani yangu. Nataka kuhamisha nguzo ije karibu na uzio wa nyumba ninayoishi. Gharama ya kuihaisha nguzo kutoka barabarani ni yangu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…