Msaada wa namna ya kutunza nywele

Msaada wa namna ya kutunza nywele

structuralist

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2012
Posts
1,230
Reaction score
907
Nimekuwa nikiwa na nywele ndefu (kichwani) kwa muda mrefu tu hasa kutokana na nature ya kichwa changu.

Sasa nywele mara ziwe ngumu mara zifubae rangi. Sasa kwa wale watalamu wa nywele ni mafuta gani mazuri ya kulainisha nywele pamoja na kuhifadhi rangi nyeusi ya nywele kutokufubaa?
 
Jaribu venus ni mazur yanaweza kuwa solution.
 
Jaribu Afro American

Pia zingatia steaming angalau kila baada ya wiki mbili

Kuosha/set kila week

Na usuke angalau mara 3 kabla hujaritach
 
Jaribu Afro American

Pia zingatia steaming angalau kila baada ya wiki mbili

Kuosha/set kila week

Na usuke angalau mara 3 kabla hujaritach
Ahsante sana. Ila hapo kwenye kusuka kuset na steaming nadhani kwa wa dada. Tatizo la afro American ni kuwa inachafua sana hata ukivua tishet tyari inakuwa ni ishu.
 
Nilipaka black, dah nilijuta. Ngozi ya kichwa yote ilikuwa ikiwasha hasa,kichwa kikawa kinauma haswa mara shingo na pajila uso kukavimba kulala kukawa ishu yani ilikuwa ishu. Nimesema SITORUDIA TENA kama nywele zitakuwa za njano ts ok lakini sio kwa black
 
Jaribu Afro American

Pia zingatia steaming angalau kila baada ya wiki mbili

Kuosha/set kila week

Na usuke angalau mara 3 kabla hujaritach
Mimi upara unakuja kwa kasi naomba msaada, nitumie hair product gani kuzuia huo upara?
 
Mimi upara unakuja kwa kasi naomba msaada, nitumie hair product gani kuzuia huo upara?
 
Nimekuwa nikiwa na nywele ndefu (kichwani) kwa muda mrefu tu hasa kutokana na nature ya kichwa changu.

Sasa nywele mara ziwe ngumu mara zifubae rangi. Sasa kwa wale watalamu wa nywele ni mafuta gani mazuri ya kulainisha nywele pamoja na kuhifadhi rangi nyeusi ya nywele kutokufubaa?
Mpendwa ! ukitaka kutunza na kuzistawisha nywele zako Naturally basi tumia kwa kupakaa Yourgat (maziwa ya mgando) mara 2 kwa wiki !! utaona tija la urembo wa nywele.
good Luck
 
Wakuu mi hii ni mara yingi na mpaka mida hii natumia super black kwa nywele zangu na je inaweza kuwa na madhara yoyote kichwani na mwilini kwa ujumla..??? naomba msaada kwa wanaoelewa na hasa nn mbadala wa super black nataka niachane nayo maana nimeanza kuichoka mpaka saivi

Msaada pleease kwa wale walio na uelewa.....!!!
 
Nywele ndefu tabu sana, Mi ni low cut tu hata kitana sinaga
 
tatizo mi nywele zangu ziko kama za Jason Stantham sijui nifanyaje ili nywele zijae dah!
 
Mpendwa ! ukitaka kutunza na kuzistawisha nywele
zako Naturally basi tumia kwa kupakaa Yourgat (maziwa ya mgando) mara 2 kwa wiki !! utaona tija la urembo wa nywele.
good Luck
Ahsante sana mkuu hiyo nitaijaribu ila ina namna ya kutumia au unachukua tu maziwa kasha unasugulia kichwani?
 
Back
Top Bottom