hbi
JF-Expert Member
- Feb 6, 2011
- 678
- 298
Ndugu wanajamvi, naomba mtu yeyote anaeweza kutusaidia juu ya hili suala, tunaambiwa pindi tumalizapo elimu zetu tujiajiri wenyewe.. Ni jambo zuri ila tatizo linakuja kwenye namna ya kujiajiri.. Tulio wengi huwa tunawaza kufanyaa biashara na baadhi yetu tunadhani kua biashara ni kuuza bidhaa au kufungua maduka makubwa.. Lakini tukiangalia upande mwingine je kunauwezekano wa mtu kufanya biashara kulingana na taaluma yake? kwa mfano mwalimu,mhasibu,mhandisi,mtu wa kompyuta na wengine wengi.. Mwenye ufaham wa hii kitu naomba atusaidie ili tuweze kujikomboa na janga hili la taifa