DEREVA WA UDA
New Member
- Apr 27, 2014
- 4
- 0
Mimi ni dereva wa UDA.kwa niaba ya wenzangu nimeona nijitokeze ili tupate msaada wa kisheria kwa mambo yafuatayo (1)Tunaendesha magari kwa saa 18 mfululizo siku mbili halafu unapewa siku moja ya kupumzika.nina maana ukianza kazi saa 11 alfajili mpaka saa 4:30 usiku mpaka ukajaze mafuta na kulipa hela za hesabu itakuwa kama saa 6 usiku.ukisema urudi nyumbani kama unakaa mbali hutaweza inabidi ulale kwenye gari kwa ajili ya kuamka alfajili ya saa 11 kuanza kazi tena.ambapo siku inayofuata ndio utapumzika.kwa maana hiyo tunafanya kazi masaa 18 halafu tunapumzika masaa 4 kisha tunafanya masaa 18 harafu ndio tunapumzika siku inayofuata.Ndio sababu ukiziona gari nyingi za hii kampuni zimepigwa pasi hii ni kwa ajili ya usingizi (2)tunalipwa 150000 wanakata nssf 15000. Inabaki 135000 ukiwa hukutimiza hesabu katika siku zilizopita inakatwa unajikuta mwisho wa mwezi huna kitu. Mawazo ya kukosa mshahara+ haraka ya kutafuta hesabu+usingizi wa siku mbili = ajari. Ndio maana ukiziona hizi basi lazima zimegongwa. Hatujipendei (3)Tulikuwa tumefikili kujiunga na chama cha wafanyakazi cha COTWU ili kutetea haki zetu. Lakini walipokuja hata hatujui walijibiwa nini maana nao waliingia mitini mpaka leo. yako mengi lakini haya ni machache tu. Tunaomba msaada wenu wadau wa jf.