Msaada wa sheria kwa madereva wa UDA

DEREVA WA UDA

New Member
Joined
Apr 27, 2014
Posts
4
Reaction score
0
Mimi ni dereva wa UDA.kwa niaba ya wenzangu nimeona nijitokeze ili tupate msaada wa kisheria kwa mambo yafuatayo (1)Tunaendesha magari kwa saa 18 mfululizo siku mbili halafu unapewa siku moja ya kupumzika.nina maana ukianza kazi saa 11 alfajili mpaka saa 4:30 usiku mpaka ukajaze mafuta na kulipa hela za hesabu itakuwa kama saa 6 usiku.ukisema urudi nyumbani kama unakaa mbali hutaweza inabidi ulale kwenye gari kwa ajili ya kuamka alfajili ya saa 11 kuanza kazi tena.ambapo siku inayofuata ndio utapumzika.kwa maana hiyo tunafanya kazi masaa 18 halafu tunapumzika masaa 4 kisha tunafanya masaa 18 harafu ndio tunapumzika siku inayofuata.Ndio sababu ukiziona gari nyingi za hii kampuni zimepigwa pasi hii ni kwa ajili ya usingizi (2)tunalipwa 150000 wanakata nssf 15000. Inabaki 135000 ukiwa hukutimiza hesabu katika siku zilizopita inakatwa unajikuta mwisho wa mwezi huna kitu. Mawazo ya kukosa mshahara+ haraka ya kutafuta hesabu+usingizi wa siku mbili = ajari. Ndio maana ukiziona hizi basi lazima zimegongwa. Hatujipendei (3)Tulikuwa tumefikili kujiunga na chama cha wafanyakazi cha COTWU ili kutetea haki zetu. Lakini walipokuja hata hatujui walijibiwa nini maana nao waliingia mitini mpaka leo. yako mengi lakini haya ni machache tu. Tunaomba msaada wenu wadau wa jf.
 
dah!" hilo la kupgwa pasi ni kweli, ndio mana nilikua najiuliza unakuta gar mpya ila ina pasi za kutosha.
 
Wenye msaada njoeni huku!
Kwenye huo mshahara pia ni janga la wanaharakati!
Maana nchi hii sasa ina wanaharakati na wachumia tumbo!
 
Kwasababu ya usingizi ukitaka kujue tuchunguze kwenye foleni au trafic right gari ikisimama kama dakika mbili lazima usinzie hapo unamtegemea konda akuamshe.akiwa bize abilia lazima utasikia oyaa! We dereva vipi?
 
kani UDA mnaambia mpeleke hesabu ya sh ngapi? na inapishana kiasi gani na za magari mengine yenye ukubwa kama huo? ila pia bado mna advantage ya kulipwa mshahara tofauti na hesabu mnayopeleka. pili kama mnalipwa mshahara lazima uanzie kweny kima cha chini cha serkiali ambapo ni zaidi ya 170,000. pia maisha ni vita madereva wengine hawana cha kupumzika na wewe kama unapewa siku moja ya kupumzika, mshahara na bado unabaki na chenji kwani vyovyote vile hesabu inafika na kama inapungua ni mara moja moja. imgekuwa wanawanyanganya magari kabla ya hesabu ingekuwa ngumu lakini kama mumewekewa hesabu wewe ikifika unapeleka gari au vipi unajipatia na haki yako ya ziada kosa liko wapi?
 
nakumbuka hapo kuna chama cha wafanyakazi (cotwu) ingawa nacho kimechoooooka , anzia hapo huku hakuna msaada wa kisheria.
 
Asante balacuda kwa kujumuika na mimi.Hesabu ni sh200000.Hela ya kuosha gari ni sh5000 na mafuta ujaze.na mafuta kwa siku unaweza ukajaza ya sh 165000 kwa hiyo jumla kama sh 370000.mshahara wetu ni sh150000 ukikatwa nssf inabaki sh 135000 ukipiga pasi gari mshahara hakuna wote wanakata.magari mengine kwa mfano kuna muhindi mmoja ana eicher kama hizi hesabu ni sh120000 mafuta wanasema wanaweza jaza ya 80000 wao hawatoi hela ya kuoshea gari.kwa siku anatakiwa atafute sh 200000 tu ya boss zinazozidi zake.na mshahara ni sh 200000 kwa mwezi.na ikitokea amepiga pasi gari hakatwi kampuni inatengeneza.nakuna dereva wa kuja kumpokea kila siku ili apumzike kwa masaa kama manne
 
Hao cotwu walikuja halafu wakaingia mitini.sasa sijui walikatiwa kitu kidogo wakae kimya au walipigwa mkwala waache kufatilia mambo ya watu. Wote hatufahamu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…