msaada wa sheria plz

msaada wa sheria plz

kithumn

Member
Joined
Feb 13, 2013
Posts
12
Reaction score
1
Ninakesi ya madai iko mahakama ya wilaya ilala,msimamizi wa mirathi ameuza kiwanja cha mirathi,baada ya kupeleka malalamiko mahakani anasema alishafanya mgawo wakati sio kweli,inventory anasema cop kapoteza na fail alilofungulia mirathi halopatikaniki mahakamani,naomba mnisaidie je baada ya msimamizi kufail inventory ndo fail linafungwa?,au hadi afail account?
 
Ninakesi ya madai iko mahakama ya wilaya ilala,msimamizi wa mirathi ameuza kiwanja cha mirathi,baada ya kupeleka malalamiko mahakani anasema alishafanya mgawo wakati sio kweli,inventory anasema cop kapoteza na fail alilofungulia mirathi halopatikaniki mahakamani,naomba mnisaidie je baada ya msimamizi kufail inventory ndo fail linafungwa?,au hadi afail account?
samahani, huyo ni msimamizi wa mirathi aliyeteuliwa na mahakama? kama aliteuliwa na mahakama lazima kuna jalada la mirathi litakuwa lilifunguliwa kule mahakamani. pia, yeye lazima atakuwa alipeleka orodha ya mali zote ambazo marehemu alikuwa anamiliki ambazo zilitakiwa zigawanywe katika mirathi. kwa kawaida, anatakiwa pale tu atakapomaliza kugawa mirathi, arudi mahakamani ili akaonyeshe ushahidi wa namna gani amegawa, na jalada la mirathi lifungwe.

kama amefuja mali, ametapanya mali n.k, mahakama itamwajibisha na atazilipa zote alizofuja au kusababisha hasara isiyo na sababu. kama anasema amefanya mgawo kumbe sio kweli, anasema amepoteza copy ya inventory, na file alilofungulia mirathi halipatikani mahakamani, nafikiri huo ni ushahidi mzuri tu kuthibitisha kuwa huyo anatakiwa kuadibishwa na kulipa mali alizofuja. nenda kwenye mahakama iliyomteua ili utoe maelezo hayo na watakushauri nini cha kufanya.

lakini inavyoonekana, inaonekana kana kwamba hadi watu wa mahakamani wamehusika katika kulaghai, itakuwaje jalada alilofungulia mirathi lipotee, yeye hana copy ya inventory, pia ninyi hamjapata mgao......mbona kuna mazingira kama kuna chain ya watu zaidi ya mmoja wameshiriki kulaghai na kujaribu kupoteza ushahidi? kama wewe ni legal heir, haujapata mgao na yeye anasema amegawa, basi itabidi athibitishe mahakamani amekugawia nini. NENDA KWENYE MAHAKAMA ILIYOMTEUA utaambiwa nini cha kufanya, ukishindwa huko, ndio uende legal and human rights centre pale watakusaidia, uende kwa mawakili wa kujitegemea wowote wale (kwa fees) watakusaidia, n.k. nimeandika nikiwa na haraka, nikitulia nitaandika vizuri na kwa kutulia zaidi. pole sana.

View attachment 103047
View attachment 103047

View attachment 103048View attachment 103048View attachment 103048View attachment 103048
 
Back
Top Bottom