samahani, huyo ni msimamizi wa mirathi aliyeteuliwa na mahakama? kama aliteuliwa na mahakama lazima kuna jalada la mirathi litakuwa lilifunguliwa kule mahakamani. pia, yeye lazima atakuwa alipeleka orodha ya mali zote ambazo marehemu alikuwa anamiliki ambazo zilitakiwa zigawanywe katika mirathi. kwa kawaida, anatakiwa pale tu atakapomaliza kugawa mirathi, arudi mahakamani ili akaonyeshe ushahidi wa namna gani amegawa, na jalada la mirathi lifungwe.Ninakesi ya madai iko mahakama ya wilaya ilala,msimamizi wa mirathi ameuza kiwanja cha mirathi,baada ya kupeleka malalamiko mahakani anasema alishafanya mgawo wakati sio kweli,inventory anasema cop kapoteza na fail alilofungulia mirathi halopatikaniki mahakamani,naomba mnisaidie je baada ya msimamizi kufail inventory ndo fail linafungwa?,au hadi afail account?