Msaada wa sheria wanajamii.

Msaada wa sheria wanajamii.

mpoki2086

New Member
Joined
Jan 10, 2013
Posts
1
Reaction score
0
Hivi raisi anapoteua jaji anakua anamfahamu au anateua kwasababu katiba ina mpa mamlaka? Nakama ni kweli mbona kwenye case ya lema chande alijitoa akidai anintres na case.
 
Tafadhali rejea upya sababu ya CJ kujitoa katika kesi ya Lema hiyo uliyoitaja ni upotoshaji.
 
Hivi raisi anapoteua jaji anakua anamfahamu au anateua kwasababu katiba ina mpa mamlaka? Nakama ni kweli mbona kwenye case ya lema chande alijitoa akidai anintres na case.

Kuna tofauti kati ya mtu kuteuliwa kuwa jaji na jaji kupangiwa kesi za kuamnua.

Rais ndiye anayeteuwa watu kuwa majaji. Lakini Rais hawapangii majaji kesi za kuamua.

Hizo kesi wanajipangia wenyewe majaji huko huko mahakamani baada ya kuteuliwa na Rais kuwa majaji.

Kama Rais angekuwa anawateuwa majaji na kuwapangia kesi za kusikiliza basi hapo kusingekuwa na uhuru wa mahakama.
 
kama tutakumbuka vyema msingi wa kuwepo mihimili mitatu ya dola (state organs) ni kuweka mazingira ya mizania (chek en balance) ili kila mhimili asiwe na uhuru wa kupitiliza kuepuka ulevi wa mamlaka. ndo maana ili raisi awe halali lazima aapishwe na jaji mkuu, na jaji mkuu nae anateuliwa na raisi. kimsgi lengo siyo kuwa na mamlaka juu ya mhimili mwingine ndo maana jaji akishamwapisha raisi hampangii namna ya kufanya kazi hivyo hivyo jaji hapangiwi namna ya kuongoza mahakama, uteuzi wa jaji au hakimu wa kusikiliza kesi ni kazi ya mahakama zenyewe siyo shinikizo la mtu nje ya mahakama husika.
 
Back
Top Bottom