kama tutakumbuka vyema msingi wa kuwepo mihimili mitatu ya dola (state organs) ni kuweka mazingira ya mizania (chek en balance) ili kila mhimili asiwe na uhuru wa kupitiliza kuepuka ulevi wa mamlaka. ndo maana ili raisi awe halali lazima aapishwe na jaji mkuu, na jaji mkuu nae anateuliwa na raisi. kimsgi lengo siyo kuwa na mamlaka juu ya mhimili mwingine ndo maana jaji akishamwapisha raisi hampangii namna ya kufanya kazi hivyo hivyo jaji hapangiwi namna ya kuongoza mahakama, uteuzi wa jaji au hakimu wa kusikiliza kesi ni kazi ya mahakama zenyewe siyo shinikizo la mtu nje ya mahakama husika.