Msaada wa Sheria ya Ardhi (Ya Kiswahili) - Sura ya 89

The Giant

JF-Expert Member
Joined
Jun 24, 2012
Posts
504
Reaction score
96
Ndugu Wanasheria,

Kuna mwekezaji anataka amwodoe bibi yangu akidai kuwa eneo ni lake( na ikiwa sivyo Mwekezaji kaja 2011. Na bibi kanunua eneo hilo tangu 1990 na yuko mbali na mwekezaji.).

Kesi ipo mahakamani, bibi kaomba msaada ajue kinachoendelea, kuna mheshimiwa kampatia kitini cha sheria ya ardhi sura ya 89.

Kimeandikwa kwa kiingereza, hawezi kukisoma na Mimi kumtafsiria sina ujuzi huo na nnaofia ntapindisha kilichoandikwa.

Naomba msaada kama naweza kupata cha kiswahili ili Bibi ajue kichoendelea na aweze kupigania haki yake ya kutonyang'anywa Mali yake.

Natanguliza shukrani.
 

Attachments

  • DSC_1160.jpg
    55.5 KB · Views: 60
Mkuu shaeria hiyo (sura ya 89) haina tafsiri rasmi katika lugha ya kiswahili. Chakufanya tafta mtu mwenye ujuzi amtafsirie sheria hiyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…