CHUAKACHARA
JF-Expert Member
- Jun 3, 2011
- 12,357
- 6,424
Wapendwa naomba msaada wa hili. Nilinunua shamba, mwanaukoo akataka kulikomboa (redeem a clan shamba). Akaambiwa kuwa alipe laki saba. Hakimu hakuweka hizo hela zilipwe ndani ya muda gani. Imepita kama miaka 5 , leo ameibuka eti anataka kulipa. Je sheria inasemaje katika scenario kama hiyo.
Asante.
Miaka 12 ingekuwa sahihi kwenye issue ya shamba tu, lakini hapo issue iliyopo ni kulipa deni maana issue ya ardhi ishakuwa settled, ndio maana nikamuomba aje na condition ya ya malipo ya hilo deni, na je ndani ya hiyo miaka mitano yeye mleta mada alichukua hatua gani kudai deni lake?,Kwa mujibu wa Sheria ya Muda wa Ukomo naona bado yuko sahihi kwa sababu madai yoyote kuhusu kurejeshewa shamba ukomo wake huwa ni miaka 12 tangu pale mgogoro ulipoibuka.