Mkuu Ngambo Ngali,
Mimi natofautiana na wewe kwa suala dogo kwamba hiyo fire extinguisher ni kwa faida yako na ni tahadhari kabla ya hatari ya moto kutokea. Ni heri ukanunua hiyo FE kwa kuwa hiyo risiti ya faini haitakusaidia kuzima moto endapo utatokea kwenye gari lako. Yatupasa kufahamu kwamba moto unaweza kudhibitiwa kwa urahisi ndani ya dakika kumi tu za mwanzo. Na yatupasa kufahamu kuwa kazi ya polisi wote pamoja na hawa wa barabarani ni kuhakikisha sheria tulizojiwekea tunazifuata kwa usalama wetu na mali zetu.