Msaada wa swali hili tafadhali

Msaada wa swali hili tafadhali

Wababa13

Senior Member
Joined
Dec 27, 2017
Posts
105
Reaction score
70
Habari zenu wote,

Naomba kuuliza kwa mfano umekutana swali hili hapa “Eleza ni njia gani utatumia ili kufanikisha zoezi la uhesabiji wa SENSA linalo endeshwa kijijini/mtaani iwapo wananchi wameligomea?”.

Naomba msaada wa majibu ya swali hilo chukulia ndo wewe umekutana nalo kwenye interview ya kumtafuta Afisa Mtendaji wa Kijiji/Mtaa.

Nasubiria majibu yenu mazuri.

IMG-20220605-WA0000.jpg
 
Nitatoa elimu , kuhusu faida na umuhimu wa sensa kwa watu waliogomea sensa...nitawashawishi mpaka twende sawa zoezi liendelee....nitafanya vikao na mikutano nikishirikiana na viongozi wa kijiji au mtaa ili kufanikisha elimu kuwafikia wote
 
Nitatoa elimu kuhusu sensa, nikijikita haswa kwenye faida za sensa katika muktadha wa maendeleo na huduma za kijamii.

Elimu itatolewa kupitia mikutano ngazi ya mitaa au vitongoji kwa kushirikiana na viongozi wa eneo husika na raia wanaoishi eneo husika wenye uelewa mpana kuhusu sensa.

Mikutano hiyo itawapa pia fursa wananchi kuuliza maswali na watapata majibu.

Pia nitatoa fursa kwa yule ambae anahisi anasababu binafsi za kugomea sensa na hayuko Tayari kuweka wazi kupitia mikutano basi afike ofisini kwa majadiliano zaidi kuhusu hoja zake.
 
Back
Top Bottom