Nitatoa elimu kuhusu sensa, nikijikita haswa kwenye faida za sensa katika muktadha wa maendeleo na huduma za kijamii.
Elimu itatolewa kupitia mikutano ngazi ya mitaa au vitongoji kwa kushirikiana na viongozi wa eneo husika na raia wanaoishi eneo husika wenye uelewa mpana kuhusu sensa.
Mikutano hiyo itawapa pia fursa wananchi kuuliza maswali na watapata majibu.
Pia nitatoa fursa kwa yule ambae anahisi anasababu binafsi za kugomea sensa na hayuko Tayari kuweka wazi kupitia mikutano basi afike ofisini kwa majadiliano zaidi kuhusu hoja zake.