Msaada wa tafisiri

BABA CHANJA

Member
Joined
May 23, 2013
Posts
75
Reaction score
7
Wataalam wa lugha Naombeni msaada wa tafisiri ya neno hili
"Unlock your potential"
 
potential ni uwezo alionao mtu ambao haujaonekana bado

na ku unlock ni kufungua...

ni sawa na kusema fungulia kipawa chako au uwezo wako
 
Asante sana 'The Boss'! Nilikuwa ninatafuta tafsiri ya 'potential'. Ulieleza vizuri sana. Sasa, je unaweza kunisaidia na hatua moja zaidi, yaani, kutafsiri sentensi hii?
'Daudi has a lot of potential'
Asante!
 
Daudi ana vipawa vingi.

Mchezaji mzuri w soka.
Mtaalamu wa hesabu
Anachora picha nzuri sana
Ni mzuri wa kujenga hoja

Kwa maana kwamba akifuunguka anaweza;
kucheza soka la kulipwa,kuwa Professor wa Chuo kikuu,akatokea kuwa Msanii mzuri na hata kuwa Kiongozi au mwanasiasa mahiri/mzuri.
 
Nafikiri 'Daudi ana vipawa vingi' hutafsiriwa 'Daudi is very gifted / talented.' Lakini 'Daudi is very gifted (au 'Daudi has a lot of talent/gifts)' ina maana tofauti kabisa na 'Daudi has a lot of potential' kwa Kingereza. Labda hamna tafsiri ya moja kwa moja. 'The Boss' alisema sawa hapo juu alivyosema 'potential' inahusu 'uwezo alionao mtu ambao haujaonekana bado'. Kwa 'Daudi ana vipawa vingi', tayari umeshaona vipawa vyake (at least kwa kiasi) - vipawa tayari ni wazi kwa watu. Hiyo siyo maana ya 'potential'. Lakini labda ninakosa kwa kiasi - mimi ni mwingereza na ninajitahidi kujifunza Kiswahili!
 
kwa tasri sisi au ya neno kwa neno ni "fungua uwezo wako"
kimaana(onesha uwezo wako)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…