"Columnist" ni mwandishi ayaandikaye makala gazetini, kwa kawaida ayaandika hayo makala kila wiki au kila siku. Mzizi wa neno ni "column", kwani ufafanuzi mmoja wa "column" ni makala mafupi yaandikwayo kila wiki au siku.
"Pattern" ni neno lenye fafanuzi nyingi. Nomino au hata kitenzi. Kwa mfano:
Pattern = Bombwe
The curtain was decorated with patterns. = Pazia lilipamba kwa mabombwe.
Pattern = Ruwaza
I drew the diagram according to the pattern. = Nilichora ramani kulingana na ruwaza.
Pattern = Utaratibu
His steps followed his usual pattern. = Hatua zake zilifuata utaratibu wake wa kawaida.
Ukinipa sentensi ya mfano ya Kiingereza, nitaweza kuboresha tafsiri.
Niseme, mimi ni mwanafunzi wa Kiswahili tu - na omba radhi kwa Kiswahili changu si kizuri.