Msaada wa tafsiri tafadhali

comperano ....ladha ya kweme inafanana na nini?

Ladha ya kweme ni sawa na kama zilivyo jamii nyingi za karanga na pengine nazi...inatumika sana katika kupikia chakula kama mafuta/karanga
 
Yaani wanaliita oysternut kwa kuwa umbo lake limefanana na oyster shell ya baharini - ukilikata/ukilivunja kiutaalamu linafunguka kama oyster shell...utamu wake ni kama wa karanga, ila zina mafuta sana...
 
Fenesi ni Jack fruit,
Thanks in Advance ni " Natanguliza Shukrani" ukipenda ongeza Shukrani zangu
 
asanteni kwa ufafanuzi wa hizo kweme karanga
 
Hivi wana JF neno Kiosk ni kiswahili ama ni kiingeretha?

kiosk ni neno la kiingereza ambalo limetumika kwa muda mrefu katika kiswahili lakini kwakuwa lugha hukua neno sahihi la kiosk kwa kiswahili ni KIBINDO.neno limezaliwa kwa kuchukua herufi za mwanzo yaani KI-kibanda cha BI-biashara,NDO-ndogondogo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…