Msaada wa tafsiri ya warning light hii kwenye Suzuki Carry (Kirikuu)

Dafo

Member
Joined
Aug 1, 2012
Posts
75
Reaction score
69
Wakuu habari za asubuhi,

Tafadhali naomba msaada nilikuwa naendesha Suzuki Carry (kirikuu) lakini ghafla ikawasha hiyo warning light kwenye dashboard. tafadhali naomba kuelewa hiyo taa inamaanisha shida iko eneo gani au shida ni nini kabla sijaenda kwa mafundi wetu?

 
Hivi kuna njia ya kurudisha hiyo kitu kama imetolewa?
Madhara ya kutorudisha ni yapi?

Kwa gari za zamani haina madhara sana. Ila kwa gari za kisasa utaichukia gari yako.
 
Reactions: RR
Umejibu swali moja mkuu.
Madhara yake ni yapi hasa?
Inarudishika?
Madhara yapo kwenye mafuta.

Catalytic converter inafanya content ya moshi kuwa Carbon dioxide na maji. Hii inasaidia sana kutochafua mazingira.

Bila Catalytic converter gari yako itakuwa inaemmit Carbon monoxide(CO), Hydrocarbon(HCO) pamoja na Oxygen gas.

Uwepo wa Oxygen sensor baada ya catalytic converter inaweza kusense kwamba kiasi kikubwa cha Oxygen gas kinapita iwapo tu catalytic converter itaondolewa (rejea emission inayotoka bila catalytic converter).

Kitendo cha Oxygen gas nyingi kuwa detected kinatafsiriwa na Control Box (ECU) kwamba mafuta mengi yanaingia kwenye engine hivyo ECU itaforce mafuta yanayokuja kwenye engine yapungue (kwa kupunguza muda wa nozzle kuwa wazi).

Ndio maana gari zingine ukitoa masega lazima iwe na misfire.

Natumai umenielewa.
 
Reactions: RR
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…