Ni mwaka wa 18 sasa nasumbuliwa na tumbo linajaa gesi na kuunguruma sana hadi naogopa kukaa na wenzangu. Cha ajabu pia hata mwili ukipata joto kiasi cha kutoa jasho nahisi kuchomwachomwa mwili mzima mithili ya mtu aliyeng'atwa na siafu.
Nimezunguka hospitali nyingi hadi Muhimbili lakini naambiwa sina tatizo,sijui nifanyeje.Baada ya Muhimbili nilienda hapo kwa hao watu wa NATURAL THERAPIES CENTER nao wakala hela zao lakini wapi.
Ushauri please!