1.Hiyo amoeba ilikua diagnosed vipi na wapi? Huwa unapata dalili zipi na kufanyiwa kipimo kipi (na wapi) kuambiwa una amoeba?
2.Huwa unamaliza dozi ya dawa unazoandikiwa?
3.Ni kwamba baada ya kutumia dawa unapata nafuu, kisha baada ya muda (muda gani?) unaanza kupata tena upya hizo dalili, au ni kwamba dawa hazijawahi kukupa nafuu yoyote?- Hapo kuna mawili, kwamba ni kweli shida ni amoeba, kinachotokea ni unapata amoeba, unatibiwa vizuri na kupona, kisha unaendelea na tabia zako zile zile hatarishi zilizokufanya upate amoeba (eg kunywa maji yasiyochemshwa, kula chakula kilichopoa au ambacho hakijapikwa vizuri, kula chakula/matunda bila kunawa mikono, kupenda kula kachumbari ambayo huna uhakika kama nyanya zake zilioshwa vizuri na kwa usahihi, etc etc); So,hapo inakua hakuna namna zaidi ya kupata amoeba upyaaaa,
AU hiyo sio amoeba bali ni tatizo la tumbo ambalo linahitaji ufanyiwe vipimo beyond stool analysis kujua shida na upatiwe matibabu stahiki (hasa kama huwa hupati nafuu yoyote hata baada ya kutumia dawa).
Ushaur wangu:
Kwa maoni yangu, kitu cha kwanza kwa sasa hivi cha muhimu kabisa ni kudetermine je, kinachokusumbua ni amoeba kweli? Na hapa ni lazima na muhimu uonwe na kuwa attended na daktari bingwa (wa magojwa ya ndani-physician) kwenye hospitali ya rufaa yenye uwezo wa kufanya vipimo beyond stool analysis (vipimo kama stool culture,etc kulingana na dalili zinazokukabili).
Pole sana mkuu. Wahi haraka hospitali ya rufaa ya mkoa au hospitali ya kanda yenye physician upate muafaka. Ni muhimu sana hii...Unaweza ukawa kila siku unatibiwa "amoeba" ambayo haipo kumbe una tatizo kubwa kwenye utumbo linaendelea kukukula tuu (naongea hivi kwa uzoefu wangu-mtu anatibiwa amoeba miaka na miaka haponi, kumbe ana saratani au uvimbe kwenye utumbo).
JOESKY