Habari wana JF,
Naomba msaada kwa mwenye uelewa au mwenye uwezo wa kunifanyia searching, Ndugu yangu ana
tatizo la macho linaitwa Gene Therapy, retinits pigmatos, kwa ufupi tu tiba hii Tanzania hakuna.
Sasa msaada ninaohitaji kwa mwenye uelewa hasa kwa nchi zilizoendelea kama kuna Hospital.taasisi/clinic yoyote katika nchi zilizoendelea inayotoa tiba hii, kwa sababu mara ya mwisho nilifuatilia nchini Ujerumani nikaambiwa bado wanafanya utafiti wa tiba ya ugonjwa huu wa macho.
Huyu ndugu yangu ni kama nusu kipofu anapata shida sana, naomba mchango wenu wadau kama kuna mwenye ufahamu tiba hii inapatikana wapi.
cc:
Riwa