Msaada wa tofauti kati ya maonesho na maonyesho

Msaada wa tofauti kati ya maonesho na maonyesho

matyhans

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2013
Posts
611
Reaction score
403
Jaman naomba msaada wa tofauti kati ya maonesho na maonyesho
 
Nenda balaza la kishwahili Tanzania, nazani wana majibu mazuri. na mimi naomba unisaidie kuwauliza tofauti kati ya NAZANI na NADHANI.
 
Maonesho linatokana na Ona, Onesha: fanya kitu kionekane
Maonyesho linatokana na Onya; kumrekebisha mtu aliyekosea, kumtia adabu, kumtahadharisha na hatari fulani.

*Lakini kwa sababu lugha hubadilika kutokana na kupita kwa wakati pamoja na mazingira, watu hutumia Maonyesho kumaanisha Maonesho.
Tofauti kati ya Nadhani/Nazani, Dhambi/Zambi, Thelathini/Selasini, Themanini/Semanini, Tafadhali/Tafadhali, tofauti zote hizo husababishwa na mazingira au watu kutozingatia sana sheria za lugha. Kuna watu wengi wana tatizo na matamshi yenye, "dh", na "th".
Kuna msemo wa Kiswahili, "Mazoea hujenga tabia"
 
maonesho linatokana na ona, onesha: fanya kitu kionekane
maonyesho linatokana na onya; kumrekebisha mtu aliyekosea, kumtia adabu, kumtahadharisha na hatari fulani.

*lakini kwa sababu lugha hubadilika kutokana na kupita kwa wakati pamoja na mazingira, watu hutumia maonyesho kumaanisha maonesho.
Tofauti kati ya nadhani/nazani, dhambi/zambi, thelathini/selasini, themanini/semanini, tafadhali/tafadhali, tofauti zote hizo husababishwa na mazingira au watu kutozingatia sana sheria za lugha. Kuna watu wengi wana tatizo na matamshi yenye, "dh", na "th".
Kuna msemo wa kiswahili, "mazoea hujenga tabia"
nimekuelewa
 
Back
Top Bottom