Msaada wa ufafanuzi katika ujenzi wa ghorofa moja

Mkuu kama baada ya ghorofa moja nikapaua mabati badala ya kuwaga zege je gharama itafika huko 100m?
nina kiwanja Mlimani natamani hiyo ramani ya ghorofa la kupaua
Kwa standard house,ambayo may be juu ikawa na chumba na sebule na chini kuwa na vyumba Milioni 100.Inafika na kuweza kuzidi.

.Ingawaje kwa swali lako siwezi kuwa na jibu la moja kwa moja kwani inategemeana na ramani yako

Isije ikawa aina ya nyumba unayotaka juu chumba kimoja chini kimoja.hiyo inaweza isifike mil100.hahaha!
 
Mkuu kama baada ya ghorofa moja nikapaua mabati badala ya kuwaga zege je gharama itafika huko 100m?
nina kiwanja Mlimani natamani hiyo ramani ya ghorofa la kupaua
Kwa issue ya hiyo ramani,niinbox.

Tuzungumze.Nikuandalie michoro.
 
Mkuu nimekuelewa ngoja nijikusanye, maana nina kamchoro kangu nitakutumia ipo siku u-design vizuri
Kwa issue ya hiyo ramani,niinbox.

Tuzungumze.Nikuandalie michoro.
 
Mkuu nimekuelewa ngoja nijikusanye, maana nina kamchoro kangu nitakutumia ipo siku u-design vizuri
Vipi mtaalam.
Ulipata muafaka.. maana hapa nina wazo kama lako la kujenga ghorofa 1 simple la makazi. Kiwanja ninacho 522sqm flat ila hela ya kuanzia ndio ya kujichanga mdogomdogo. Yaani nikisema nianze January 2022 nadhani nitamaliza 2029 huko. Hapo ni ku assume kuwa mzima, afya tele na income iongezeke.
Ila nikiona hayo mahesabu nakata tamaa kabisa.
 
Hata mm nimekata tamaa kwa mwaka huu wa 2021
ila nitauza mashamba km mawili huko porini Mama akiwaka hela za tozo ili na mm nilale angalau juu ya nyumba hata room moja juu ya dari
si unajua tena kaburi wanachimba kwenda chini ndio tutalala maisha yetu yaliyobaki
au wenyewe mnasemaje mtabaki juu ya ardhi tu bila kwenda juu au chini?
 
Nimepiga hesabu hapa kuwa kwa mwezi ni fight atleast nipate 1.5m ya uhakika itahitaji miaka 7 yaani miezi 84 kufikisha 126m ambayo ndio kighorofa kitaonekana. Duh..
 
Mkuu kama baada ya ghorofa moja nikapaua mabati badala ya kuwaga zege je gharama itafika huko 100m?
nina kiwanja Mlimani natamani hiyo ramani ya ghorofa la kupaua

Ghorofa sio kwa ajili ya maskini.
 
Dondosha na namba yako pia tukutafute
 
Wastani wa nondo ni kiasi gani na garama za ufundi kwa stages?
1. Kuchimba msingi
2. Kufanya settings
3. Kusimamisha msingi
4. Kunyanyua
 
Mkuu Vipi kama najenga kwa awamu, awamu ya kwanza kabisa walau ikomee wapi?
 
Wastani wa nondo ni kiasi gani na garama za ufundi kwa stages?
1. Kuchimba msingi
2. Kufanya settings
3. Kusimamisha msingi
4. Kunyanyua
Mpaka kufikia kwenye msingi fundi isizidi 1.3M kama unajenga dar na kama unategemea kuendelea kumtumia kwa kazi inayofuata. Kama hutamtumia kwa kazi inayofuata mpe 1.6M

Sent from my TECNO P704a using JamiiForums mobile app
 
Umeeleza vizuri, japo kumsaidia zaidi huyu mleta mada, anahitaji ghorofa chini kasebule sio sebule na juu chumba kimoja na velanda ya kupunga upepo. Kama video inavyoonyesha.
Sasa tumkadilie, chumba 1 nguzo 4 na ngazi nondp ngapi kijana ajenge
 
Kwa issue ya hiyo ramani,niinbox.

Tuzungumze.Nikuandalie michoro.
Kwanza mshauri hapa, ushauri anaoutaka ndio avutiwe na kukupa kazi usikimbilie huko. Sie waafrika tuna tatizo kubwa.
Kuna kazi imetoka, interview ya kazi ndio hiyo hapo mleta mada katoa. Sasa Wewe unaona ulichoandika hapo ndio jibu sahihi kwa hiyo interview, kiasi kwamba akupe kazi!?! Hapo kazi watapewa waliomridhisha takwa la awali, na sie wengine wapita njia kwa majibu yako tunaweza kukupa kazi vile vile.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…