nenda kaombewe kanisani. Mungu anaponya magonjwa hata leo hivi. kama umeshindwa kwenye madawa ya kidunia, Mungu hashindwi kitu. nenda kwa pasta, mweleze hali halisi, usimfiche, mwambie unatubu, hautaendelea kukaa kwenye uzinzi wa kutokuoa tena, ufunge ndoa, Mungu atakusamehe na atakuponya. Zaburi 103 inasema, akusamehe maovu yako yote, akuponya magonjwa yako yote, that means, dhambi wakati mwingine huwa ni kizuizi kikubwa sana cha mtu kupona au kutoka kwenye tatizo fulani.
Ukitubu dhambi ukaokoka, hapo ndipo utakuwa na haki ya kumdai Mungu promise aliyosema ya kuwa, akikusamehe maovu atakuponya na magonjwa yako yote. Kumbuka, katika isaya 53, Yesu alichubuliwa kwa maovu yetu, alimwaga damu kwaajili yetu, kwa kupigwa kwake sisi tumepona, who is those "sisi", wale tu wanaompokea Yesu kama Bwana na mwokozi wa maisha yao ndio wanaopata neema iliyoletwa na Kufa kwa Yesu, Yesu alimaliza yote, kilichobaki ni uamuzi tu wa mwanadamu kukiendea kiti cha rehema cha Mungu ili asamehewe maovu na aponywe magonjwa.
Biblia inasema, njoni kwangu ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha,(that means, kama hautaenda kwa Yesu hautapumzishwa mizigo yako) yaliyokushinda wewe Yesu anayaweza, madawa yameshindwa Yesu hashindwi kitu. it is your free will, democrasia ya Mungu, our God is always democrat, halazimishi mtu, ameweka mlango wa baraka na wa laana, changua kutenda mema upata baraka, ukitenda mabaya utapambana na laana. Hivyo, just decide today, jaribu, onjeni muone ya kuwa Bwana yu mwema, hata kama bado mna wasiwasi, onjeni basi.
NENDA KAOKOKE, OKOKA KIKWELIKWELI, JIUNGE NA KANISA LINALOHUBIRI WOKOVU, halafu angalia kama Mungu hatakufanyia kitu. I tell you, nimeona watu wengi wakibadilika kutoka kwenye magonjwa ya ajabu, wanapona kabisa, nimeshuhudia mengi. Mungu akusaidie uone ya kuwa, MUNGU ANAKUPENDA SANA, TENA SANA, HATAKI UUMIZE MOYO NA UO UGONJWA, NDIO MAANA YESU ALIKUFA KWAAJILI YAKO. But God can not do more than what he already did, alimaliza kila kitu pale msalabani, kilichobaki ni sisi kukisogelea kiti chake cha rehema, kusamehewa dhambi na kuponywa magonjwa.
Inawezekana umeshaenda kwenye makanisa kuombewa tayari, kwasababu gono la miaka mitatu ni mingi, na ni hatari kwa kijana kama haujaoa, kwasababu moja ya magonjwa yanayoua kizazi kwa wanaume na wanawake ni gono, pamoja na syphilis. WAKATI MWINGINE UPONYAJI HAUWEZI KUJA KWASABABU WATU WENGINE WANAKUWA WANAFIKI, WANATAKA TU UPONYAJI LAKINI HAWATAKI KUOKOKA, kama hivyo Mungu atakuacha na tatizo hivyohivyo pengine ukiumia sana siku moja utamkumbua uokoke, wengine wanaombewa lakini wanaishi na mahawara, wengine walevi na hawataki kuokoka, sasa ukiwa unamwomba Mungu akuponye wakati moyoni haumtaki, Mungu atakuponya? ndo maana wengine wameombewa hadi wameota vipara, hakuna majibu.
wengi wa waliopona hata kwenye Bible walikuwa wanamaanisha toka moyoni, kumwamini Mungu na kuambatana naye, hapo ndo utapona. lakini ukutubu,ukaamua moyoni kumfuata Yesu, yeye ndiye aliyekuumba, anaweza kukuumba upya. Nilisoma na jamaa mmoja, aliliwa kabisa kwenye jogoo lake, yaani kuna makovu mashimomashimo, na bila aibu, akiwa anaoga kwenye bafu za public, si unajua tena shule za bodi, yaani alikuwa anatia huruma.
lakini kwa Mungu yote yanawezekana. wengi walikuwa na matatizo ya ajabu, lakini Yesu anasema kwa upole, njoni kwangu ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo nami nitawapumzisha.