Msaada wa ugonjwa sugu wa ghonorea

Nikisikia m2 anataja gono Enzi hizi za ukimwi mwili unanisisimka.

wamoro kuna Dakitari hapo juu ningekushauri u-mpm nafikiri atakusaidia sana. pole sana my broda

Dorin, tema mate chini, huyu huyo unayemwamini anaweza kulileta kwako, haya mambo si ya kushangaa omba mungu tu aendelee kukulinda.
 
Dorin, tema mate chini, huyu huyo unayemwamini anaweza kulileta kwako, haya mambo si ya kushangaa omba mungu tu aendelee kukulinda.

hivi unafikiri miaka mitatu atakuwa hajamwona tu huyo doctor unayemwamini? amekwambia ameshindwa kwa madaktari. kilichobaki aende kwa Mungu akabidhi mwili, roho na nafsi yake Mungu amtengeneze. kuna jambo Mungu anashindwa? nipe jibu..
 
Wamoro kuna vitu muhimu vya kuangalia kama kweli ni gonorrhoea, na kama ni gonorrhoea ni wadudu sugu au la au ni wadudu wa magonjwa mengine. Nakkushauri ukamowone daktari, nina imani kitu cha kwanza atachofanya mi kukuandikia vipimo vya culture and sensitivity(c/s) ya hiyo discharge yako. Majibu ya c/s yatamsaidia kujua aina ya wadudu ulio naona wanatibika kwa dawa gani.

Vinginevyo daktari anaweza kukuandikia dawa za mixed infection ya gonorrhoea,chlamydia na trichomonas vaginalis. Inawezekana una mixed infection.


 
Pole sana ndugu yangu nafikiri maelekezo aliyokupa Bwana mwamba yataweza kutusaidia sisi wenye utaalamu na tiba kukushauri cha kufanya, ila the earier the better kabla complications hazijatokea.Fanya fasta usaidiwe.
 
Mmh pole sana ndugu. Fuata tu ushauri uliopewa hapo juu na umtangulize Mungu utapona then uache kuonja onja tena bila kinga usijepatwa na pangusa. Najua hakuna kitu kinasumbua, kukosesha raha na kuumiza roho kama kupatwa na magonjwa ya huko chini.
 
Inawezekna sio Gono bali ni gonjwa flani wanaliita Genital Warts au Human Papilloma Virus (HPV) maana hii haijapatiwa tiba ya uhakika.

Kuna mkuu mmoja amekuomba uweke dalili za ugonjwa wako. Kama unaona soo, mPM tu broda!

Pole sana
 
amekwmbia dawa za hospitalini zimeshindwa. umeelewa? akimbilie kwa Mungu tu.

sijasema dawa za hospitali, nimemwamnbia aende traditional medicines... vipi bana, mbona mliobaki pale airport hamjaruka hadi leo!!!
 

Pole sana kwa Kuumwa na hayo Maradhi sugu ya ghonorea Kwa Ushauri wangu jaribu Kupata Mizizi ya Mkorosho Uchemshe na maji Unywe kutwa Mara tatu Glasi tatu za hayo maji uliyochemsha fanya hivyo kwa muda wa siku saba jaribu itakusaidia sana imewasaidia watu wengi hiyo Dawa kwa imani zako itakusaidia.

Au hii nyingine pia nzuri dawa ya huo ugonjwa wa sugu wa ghonorea upate Mizizi ya Mkunazi na Asali Safi mbichi ya nyuki hiyo Mizizi ya Mkunazi Uiweke juani kama siku tatu ikikauka twanga hiyo mizizi upate unga wake uchanganye na hiyo asali mbichi Safi kama nusu kilo upate hiyo asali mbichi safi matumizi uwe unakunywa Asubuhi mchana na usiku kutwa mara tatu ukitumia kijiko kikubwa cha kulia wali kwa kulia hiyo dawa . Tumia hiyo Dawa kwa uchache wake ni siku 7 Wingi wake ni siku 21 inshallah kwa uwezo wake Mwenyeezi Mungu utapona. Na kama bado hujapona ujuwe kuwa hayo matatizo yako yanatokana na Uchawi au Tego umetembea na Mke wa Mtu ndio maana ukienda Hospitalini huwa hayapatikani Ufumbuzi wa kuyaweza kuyatibu Maradhi yako ikiwa ndio hivyo itabidi uende kwa Wataalam wa Kienyeji wanaweza kukusaidia kuondowa hilo Tego asante sana. Huo ndio Ushauri wangu .
 
Dorin, tema mate chini, huyu huyo unayemwamini anaweza kulileta kwako, haya mambo si ya kushangaa omba mungu tu aendelee kukulinda
Dorin anajaribu kumnyooshea kidole kimoja huyu bwana kaka, anasahau vitatu vinamtazama yeye. Kama alivyosema Elnino haya mambo ni kumuomba Mola tu akuepushe nayo hayana pahala bana popote yanatua
 
jaribu Kupata Mizizi ya Mkorosho Uchemshe na maji Unywe kutwa Mara tatu Glasi tatu za hayo maji uliyochemsha fanya hivyo kwa muda wa siku saba
MM asante sana kwa ushauri unaoutoa kwa wadau hapa

Nataka kujua huo Mkunazi ndio mti wa aina gani? Binafsi siujui na wala sijui unapatikana maeneo gani ya nchi yetu. Please
 


Mbona Wamoro amepotea hajataka kuja na jibu la hayo hapo ili asaidiwe zaidi?
 
eeh!pole mwanakwetu!!hope utapata dawa!hakikisha unatumia condom kila ukijamiiana sasa na hata utakapopona!!!

Mkuu CheusiMangala hiyo Avatar yako inafaa iwe kwenye yale Mambo yenu ya kikubwa sio hapa.
 
MM asante sana kwa ushauri unaoutoa kwa wadau hapa

Nataka kujua huo Mkunazi ndio mti wa aina gani? Binafsi siujui na wala sijui unapatikana maeneo gani ya nchi yetu. Please

Mkunazi unapatikana katika Makaburi ya Kisutu wewe ukiuhutaji nenda kule Makaburi ya Kisuti kawaulize walinzi wa kule watakupatia huo Mzizi wa mkunazi unatibu maradhi mengi kwa Kiingereza unaitwa jina la ( Lote Tree ) Angalia picha yake hii chini hapa
 

Attachments

  • Lote Tree.jpg
    38.8 KB · Views: 169
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…