Msaada wa ushauri hasa kutokana na hali ngumu ya kiuchumi!!!!!!!

ufumawicha

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2014
Posts
504
Reaction score
209
Wanajf,kwanza nitaanza na kuwashukuru sana kwa mawazo yenu mazuri pamoja na ushauri!Julai mwaka huu nilikuja hapa nikiwaomba ushauri wa nini nifanye baada ya kukusanya ka shilingi 700000/=Wengi mlinishauri niaanzishe kamradi.

Nami nikaanzisha kagenge na kaduka kadogo nyuma yake.Nilipoenda TRA wakadai kwa mtaji huo kodi ni sh.318000/=kwa miezi 6.Wakadai kwa miezi ya kwanza mitatu nitalipia nusu ya hiyo yaani sh.159,000/=.Basi nikalipia hiyo pesa na kupewa Tin number.

Afisa biashara kanipa leseni kwa sh.60000/=Pango nimelipia sh.90000/= kwa miezi mitatu.Gharama za kukarabati ofisi sh.41000/=.HIVYO SH.350,000/=NDIZO ZIKO KWENYE MZUNGUKO.Hadi leo nikihesabu vitu nilivyonavyo dukani na gengeni vinaleta sh.1000000/=.Hofu yangu mauzo yameshuka toka sh.60000/= hadi sh.25000/= kwa siku.

Pia kuyumba kwa bei za vitu hasa ninavyonunua ili niuze bei inazidi kupanda kiasi kwamba nahofia kama wateja wataweza kumudu bei inayobadilika kila uchao!!WATAALAMU WA BIASHARA YA GENGE NA DUKA LA REJAREJA NJOONI HAPA MNIPE UZOOEFU WENU!!!NAOMBA KWA SABABU NIKO SERIOUS NAOMBA KAMA HUNA USHAURI PITA KIMYA SIPENDI KEJELI!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…