Kuna ndugu yangu kaishi na mume wake miaka kadhaa bila kumzalia mtoto bado wanaishi wote. Mume wake amezaa watoto wa kike na wa kiume nje ya ndoa yake. Kwa kuwa wao ni mume na mke mali zao zote zimeandikwa jina la mume mke akiamini kwamba wao ni kitu kimoja. Wote wawili mke na mume wanafanya kazi na kuchangia maendeleo yao. Swali, je hii mali waliyochuma pamoja mume anaweza kuwarithisha watoto wake aliozaa nje ya ndoa? Halafu, je mke naye akifariki ndugu zake wanaweza kupata haki ya kurithi mali za ndugu yao? Ushauri tafadhali.