MSAADA WA USHAURI; Ninataka Kuanzisha Brand Ya Nguo Kama Ilivyo WCB Wasafi, Nike, Puma, Yeezy N.K

Du kaka nakushauri fanya biashara ya pembe za ndovu tu utawin haraka
Fasta nione nikufunze mambo hayo

Na unamtaji wa sh ngapi vile
 
Ahsanteni Sana Kwa Mawazo Yenu Wadau.
 
Hili linawezekana mkuu! Mimi pia hilo wazo halipo mbali kichwani mwangu! Ni wazo zuri naamini mafanikio yapo ktk hilo! Usitishwe na hizi brand za kina JAfrican boy sijui kina Wasafi hao kuna kitu kidogo sana wanaharibu wenyew Nacho Ni "Nivae Mimi" Ku brand nguo kwa jina lako Au kwa Kutumia Jina la Group lako Ni kitu ambacho lazima kitakufelisha > Fanya hivi wasikufahamu wew Ni nani Acha kazi ijitangaze yenyewe kazi ikisha pendwa ndio tukufahamu wew ! It's very simple...Kumbuka unatakiwa umuuzie kazi yako hata Yule ambae sie rafiki wa wew
 
Nashukuru Mkuu.

- Vipi Umewahi Kupata Fununu Ambako Wao Hutengenezea Mavazi Yao ?
 
nimefanya sana hiyo kitu especially tshirts, tatizo kubwa ni quality materials hapa bongo. kama upo vzr inabidi uende china. ila ushauri anza taratibu na product moja then uipush kwn market ili kujenga hiyo brand yenyewe, sometimes ni bora kuuza brand za watu kuliko kuanza na zako from scratch kwa sababu ya umaarufu/penetration. pia ikumbukwe watz sio watu wa kukubali kitu kirahisi so hayo yote yaweke kichwani...nshaona brand za watu famous wenye kuaminika kama kp,wasafi zikibuma tatizo ni hilo la kutokubali product zetu kirahisi. pia bei hua shida kwa sababu ili upunguze bei inakubidi uproduce products nyingi kitu ambacho wengi kinatushinda kutokana na mtaji kua haba.

all the best, kumbuka mafanikio hayaji kirahisi, u must invest your energy and try out. something is better than notin.
 
Unaweza Kuwajua Hata Wazalishaji Wachache Tu Huko China Mkuu ?
 
Na hao wote uliowataja brand zao zinafahamika huko dar tena kino na baadhi ya sehemu tu.Nenda huko Rukwa,Mbeya,kigoma,Shy,Katavi,Tabora etc uone kama kuna mtu anavaa hata kama amewahi kuzisikia hizo brand.
So akili kichwani chief,kwangu mimi hio biashara Hapana.
 
Wakina Nature walikua na ile brand yao TMK WANAUME kuanzia tshirts,chupi,vitambaa vya mkononi,etc lkn waulize kama walikua wanapiga hela yoyote,zilikua zinapigwa copy mtaani tu na hakuna pesa wasanii walipata.

Masudi kipanya alianza kuuza zile tshirt zake za KP mpk akafungua maduka makubwa hapa town kuuza hizo nguo zake,cheki leo alivyochoka hakuna hata mtu anamjua kupitia hio brand yake zaidi ya uchoraji wake wa katuni.
 
Tatizo watu wengi hawajui wanataka nini Biashara ili Ifanikiwe inahita usimamizi wakutosha bila kusahau....Matangazo....Unakuwa na Brand yako then unaitambulishia BAR tu..
Unategemea matokeo gani...
Watu hawataki kuwekeza kwenye...Matangazo!
 
Tatizo watu wengi hawajui wanataka nini Biashara ili Ifanikiwe inahita usimamizi wakutosha bila kusahau....Matangazo....Unakuwa na Brand yako then unaitambulishia BAR tu..
Unategemea matokeo gani...
Watu hawataki kuwekeza kwenye...Matangazo!
Kudos boss,umemaliza kila kitu.Na mwenye akili amekuelewa chief.
 
unaweza tu.inabidi kwanza ujifunze kudesign haswa tunatumia programu za kompyuta za adobe Photoshop na adobe illustrator.

Pili ujue kutengeneza screen kwa kutumia mesh au kununua machine.

tatu ujue kuchanganya madawa na aina tofauti za rangi kuanzia za OPEC,pvc mpaka plastic sol
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…