Msaada wa ushauri

Msaada wa ushauri

Paul camp

Member
Joined
Jun 14, 2021
Posts
9
Reaction score
3
Jaman mimi ni mwanafunzi wa SUA nimeandaa project plan ya ufugaji was nguruwe ila Sina mtaji naomba mwenye ushauri wa wadau wa maendeleo (stakeholders) ambao wanaweza kunisaidia kupata mtaji naombeni ushauri wenu tafadhali eneo tayari ninalo tatizo ni mtaji wa kununua chakula Cha hao nguruwe na kujenga mabanda japo nimejenga mabanda machache hadi sasa
 
Hapa JF hatunyimani najua atakuja wa kukusaidia ,na wakati tunangojea
Nipe fomula ya kulisha nguruwe maana hapa Wana miezi 6 nawalisha tu pumba laini ya mchele nimechanganya na ya mahindi kwa mbali sana
 
Hapa jf hatunyimani najua atakuja wa kukusaidia ,na wakati tunangojea
Nipe fomula ya kulisha nguruwe maana hapa Wana miezi 6 nawalisha tu pumba laini ya mchele nimechanganya na ya mahindi kwa mbali sana
Hapo hamna unachowalisha, pumba tu??
 
Msaada wangu upo hivi.. ungana na vijana wenzako watano jichangeni mpate laki mbili na elfu hamsini.. kama ulivyosema umejenga mabanda machache Hiyo laki mbili na hamsini nunua vitoto/piglets wa kuanzia Pamoja na chakula .. nendeni halmashauri Ya maji mliopo kuna Tsh million kumi kwa kila kikundi ..

Andaeni katiba ,Tafuteni Mwanasheria ,Mkuu wa wilaya atakuja kukagua mradi wenu ukiridhisha mtapata pesa 10m au chini ya hapo.

Serikali imetenga milioni miatatu hamsini kila Halmashauri kwa ajili ya vijana kazi ni kwetu /kwenu
 
Asante kwa mawazo yako bro ila Ni ngumu kupata watu watano mnaoiva interest Kama kuanz kufuga nimeanza ila ttzo Bado cjafuga kama project yangu inavyotaka
 
Kuku wangu wa kienyeji kataga mayai kumi, kaatamia wiki mbili tu halafu kaacha kuatamia mayai. Tatizo ni Nini? Nimfanyeje ili aendelee kuatamia hayo mayai?
 
Omba mtaji na siyo ushauri, maana ushauri na maneno tupu...
 
Back
Top Bottom