Kama umri unakuruhusu na ndio kwaanza unaingia kwenye ajira, nakushauri kurudia mitihani taratibu ili kukifanya kiwe kizuri ambacho hutakionea shida kukitoa. Huko mbele uendako kwenye elimu utatakiwa uwe umefaulu masomo kadhaa kwa cheti hicho na ndipo hapo itakapokuwa taabu, lakini kama utakuwa umesawazisha kwa sasa utajikuta unapeta tu kila hatua unasonga mbele. Nakuhakikishia baadae, hutaweza kusonga mbele kielimu na cheti hicho kwa baadhi ya vyuo vyetu vikubwa, mimi mmoja wa waliokwama kwa sababu hiyo na sasa nimejichimbia kwenye kufuga wanyama maana umri umekwenda japo elimu haina mwisho, naona taabu after all the years kuanza kurudia masomo. Kila la kheri!