Kwa uelewa wangu, naweza kutumia ukwasi na utajiri kutafsiri rich na wealth.
Ukwasi unaweza kuwa na kiasi kikubwa cha pesa mkononi, ambayo usipokuwa muangalifu, inaweza kupukutika na ukajikuta katika umasikini.
Utajiri, licha ya kuwa na pesa, pia unakuwa na mali zinazozalisha kipato na kukufanya kwa hali yoyote Ile usiwe na uwezekano wa kufilisika, na utajiri au wealth unaweza kurithiwa kutoka kizazi hadi kizazi hata kama kizazi kijacho kisipotoka jasho, kitafaidika.