Msaada wa wanasheria, nini athari za kufutwa kwa uchaguzi Zanzibar ndani ya Muungano?

Msaada wa wanasheria, nini athari za kufutwa kwa uchaguzi Zanzibar ndani ya Muungano?

gps boy

JF-Expert Member
Joined
Oct 3, 2015
Posts
447
Reaction score
65
Ninaomba Wanasheria Wetu mtusaidie kutuelimisha watanzania kitendo cha kuufuta Uchaguzi Wa Zanzibar una athari gani kwa kura za Muungano kwa Rais Wa Jamhuri ya Muungano? Je Rais Wa JMT anaweza kupatika pamoja Na Ufutwaji Wa uchaguzi Wa Zanzibar?
 
Wanzibari walichovya vidole mara mbili.. Umeelewa?
Lakini pia walitumia kitambulisho kimoja, sindio. Sasa unatuambiaje upandemmoja watu wamezid na upandemwingine wapo sawa labda kama walikua navitambulisho viwili vya kupigA kura apo sawa, iyo ya kuchivya co idhu kabisa
 
mimi si mwana sheria nna mtazamo tu

zipo sababu ambazo kama zingetokea ndio kura za upande wa muungano zingekuwa halali,kama uchaguzi umeharishwa/kufutwa kwa sababu kifo cha mgombea uraisi zanzibar au chama cha siasa kujitoa kwenye uchaguzi

lakini hapa sababu ambazo zimetolewa za kufuta uchaguzi ni kuwa haukuwa wa haki na ulikuwa na mizengwe mingi,kwa sababu hizi hata kama watu walichovya mpaka vidole vya miguu mara 6 bado mazingira yalikua na mizengwe na uchaguzi haukuwa wa haki kama sababu zinavyodai.

sababu hapa ni mazingira ya kupigia kura na sio watu walitafautishwa vipi kupiga kura hizi tafauti, kura zote za zanzibar na za muungano zilipigwa katika mazingira mamoja,chumba kimoja wasimamizi wale wale kwa hio kama hapakuwa na haki ni kwa kura zote na wapiga kura wote
 
Ccm jana wamesema eti kura uraisi wa tanzania hazikuaribika,wanasema walizookota ya lowassa na magufuli hazikuwepo,wanatuona watoto kweli,hizi habari wapeleke dodoma na morogoro ambapo hawana elimu na maisha yao duni,
 
Kufuta uchaguzi Zanzibar bila kuhusisha Bara tayari umeshavunja muungano. CCM wasijitetee kwenye hoja ya kisheria ambayo iko wazi kabisa. Tulitegemea wao ndio wawemstari wa mbele kutetea muungano lakini kwa maslahi ya wachache wanauvunja wenyewe.
 
Lubuva alitwamba sisi malofa kwamba zile kura za Zanzibar hazina effect huku Tanganyika. Kwa kuwa kura za Rais kule hazifiki hata laki tano, na kwa kuwa computer za NEC zilimpa Magufuri almost kura milioni 2 zaidi ya Lowassa, then hata kama kura laki tano zote za Zanzibar angepewa Lowassa, bado Magufuri angeshinda.

Akina Lubuva wana-argue kama sisi tusiojua sheria vizuri.
 
Hatuwezi kuivika nchi demokrasia kwa uwepo wa vyama vingi ambavyo kama sanamu

"Inakera uchaguzi wa Zenji umefutwa kirahisi hata umiss tz wa Sitti ilikua ishu kuvua taji"
 
Waliounganisha huu muungano kwa kuchanganya mchanga hawa walituzidi upeo hata vizazi karne na karne vijavyo haviwezi tenganisha. Hii inamaana kwa kura moja ya mzanzibari inamaana kubwa sana. Si ktk hesabu tu kama wanavyota kutuaminish. Nizaidi ya undugu wa damu. Nizaidi ya uhusiano kiuchumi, Ulinzi na mengineyo. Maslahi binafsi yanaubomoa hakika tutajutia.
 
Lakini pia walitumia kitambulisho kimoja, sindio. Sasa unatuambiaje upandemmoja watu wamezid na upandemwingine wapo sawa labda kama walikua navitambulisho viwili vya kupigA kura apo sawa, iyo ya kuchivya co idhu kabisa

Kwa kila kituo kulikuwa na chemba ya NEC na ZEC, maafisa wa ZEC na Maafisa wa NEC, kila tume ilikuwa inafanya kazi independently.
 
Kufuta uchaguzi Zanzibar bila kuhusisha Bara tayari umeshavunja muungano. CCM wasijitetee kwenye hoja ya kisheria ambayo iko wazi kabisa. Tulitegemea wao ndio wawemstari wa mbele kutetea muungano lakini kwa maslahi ya wachache wanauvunja wenyewe.

Zanzibar washataka mamlaka kamili siku nyingi.
Na katiba yao mpya inawapa mamlaka makubwa sana..naamini kuna baadhi ya vipengele hata inapingana na ya JMT.
Ndo athari zake mnaziona sasa...kiuhalisia JMT na Z'bar ni kama nchi mbili tofauti.
 
Lakini pia walitumia kitambulisho kimoja, sindio. Sasa unatuambiaje upandemmoja watu wamezid na upandemwingine wapo sawa labda kama walikua navitambulisho viwili vya kupigA kura apo sawa, iyo ya kuchivya co idhu kabisa

Kila mzanzibari ni mtanzania,lakini si kila mtanzania ni mzanzibari!kwa maana hiyo kuna wabara wanaofanya kazi Zanzibar walimchagua rais wa jamhuri ya muungano lkn wasichague rais wa Zanzibar.
 
Back
Top Bottom