mimi si mwana sheria nna mtazamo tu
zipo sababu ambazo kama zingetokea ndio kura za upande wa muungano zingekuwa halali,kama uchaguzi umeharishwa/kufutwa kwa sababu kifo cha mgombea uraisi zanzibar au chama cha siasa kujitoa kwenye uchaguzi
lakini hapa sababu ambazo zimetolewa za kufuta uchaguzi ni kuwa haukuwa wa haki na ulikuwa na mizengwe mingi,kwa sababu hizi hata kama watu walichovya mpaka vidole vya miguu mara 6 bado mazingira yalikua na mizengwe na uchaguzi haukuwa wa haki kama sababu zinavyodai.
sababu hapa ni mazingira ya kupigia kura na sio watu walitafautishwa vipi kupiga kura hizi tafauti, kura zote za zanzibar na za muungano zilipigwa katika mazingira mamoja,chumba kimoja wasimamizi wale wale kwa hio kama hapakuwa na haki ni kwa kura zote na wapiga kura wote