Msaada wa wanasheria

Msaada wa wanasheria

Governor of Bettors-GB

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2013
Posts
10,568
Reaction score
9,710
Habari wakuu,
Kuna msaada wa kisheria unaomba kama ifuatavyo.
-Kuna Dada mmoja alichukua mkopo Bank (Ni Bank ltd fulani hivi ndogo)kama milioni tatu na nusu,kwa dhamana ya Duka na Vitu vya ndani.
Lakini pia Alimtafuta Mwezie alieweka Dhamana ya Gari.

Sasa Yule Dada baada ya muda akawa mgum kulipa na duka lake likawa kama limefilisika,na wakati huo mwezie alikuwa mjamzito na akiwa katika hatua za mwisho za Uzazi.
Sasa Kuna siku mdhamini alienda Bank kuangalia kama marejesho yamefanyika,Bank wakamfungia ndani huku akiwa na Mtoto mchanga hadi alipe deni yaani rejesho la mwezi March.Yule Dada ambae ni mdhamini akaomba msaada kwa ndugu zake wakaenda Kumlipia Rejesho kama laki nne.
Sasa mwezi uliopita Bank ikawa haimfuatilii tena yule mkopaji,wakati hadi kwake wanapajua,ikabidi wamuandame yule Mwenye gari.Na Jana tu wakaenda kukamata Gari.Kwa deni rejesho la mwezi mmoja tu.
Yule dada akaongea na ofisa mmoja,akamuambia kwamba ukija kulipa Rejesho la mwezi gari itarejeshwa.
Cha kushangaza alipoenda wakamuambia kwamba inabidi gari iuzwe kufidia deni na kumpa muda wa mwezi huku gari imezuiliwa.Na bila hata Notice yoyote

Sasa cha kushangaza ni kwamba Mkopaji hafuatwi na ndio maana inaoenakana kwamba kuna mchezo mchafu hapa.Inakuwa lengo sio kusaidia lengo ni kutengeneza mtandao wa kupata pesa kwa kuuza vitu vya watu.
Na mbaya zaidi huyo mdhamini hata Notice hajapewa.Amewaomba alipe rejesho la mwezi husika ambao ni mmoja ili gari itokea maana ndio inayomuingiza hela wao wamekataaa.
Baada ya kuwaambie kwamba inabidi mdhamini atafute mwanasheria,na wao ndio wakasema kwamba wanamfuatilia mdaiwa.
Maana wakati huohuo Mdhamini alikuwa katika utaratibu wa kufungua kesi kwa aliemdhanini.

Sasa nilikuwa nataka kupata msaada wa mwanasheria ili nimuelekeze amuone.
Lengo ni kuangalia utaratibu la pili ni kumfungulia kesi aliedhaminiwa.
 
yeye kama mdhamin ilibidi ajue kua atawajibishwa kwa kukiuka mkataba kwa anae mdhamin.kama alijiridhisha kua anaemdhamin ni mwaminif bas..lakin inapaswa yeye kama mdhamin amhimize huyo aliyemdhamin kulipa deni na anawajibu huo.
lakin pia kwa benk ni jukumu lao kujua huyo mkopaj ataweza kulipa??so lazima wakubali mali zisizo hamishika kwanza kama mfano hati ya ardhi security ya mkopo ili kujihakikishia kuwa hata mkopaji akikimbia wataweza pata haki yao kuliko kukubal vitu kama mali za dukan na vitu vya ndan.maana kama akikimbia na hakuweka mdhamin ni rahis kwao kupoteza haki yao
 
J.k
Kimechotokea katika tukio hilo ni kwamba.
Huyo Dada amekamatwa na mdhamini na yupo Mahabusu.Lakini Bank wamemuambia mdhamini ndio amdai mdaiwa.
Wao dhamana hawaachii.
Sasa hapo unakuta kwamba Polisi wamesema kwamba mdhamini haruhusiwi kufungua jalada la kesi ya Bank,inabidi afungue jalada la kwamba anamdai mdhaminiwa tu.
Sasa hapo ndio kazi,yaani Bank wametulia zao kwa kuwa wanadhamana,na unajua ni hizi Bank zetu ndogo zilizoiibuka
 
...mimi sidhani kama benki wana makosa, hasa kama ukiielewa vizuri maana ya dhamana, mambo yanapofanyika kisheria yanapaswa yamalizike kisheria, maana yake ni kwamba, kama nilichukua mkopo wa milioni mia moja nikaweka dhamana ya kitu fulani, pale nitakaposhindwa kulipa deni basi kile kitu kitanilinda kwa hiyo dhamana ni sawasawa na KINGA, bemki kisheria hawawezi kwenda kamata kitu kingine wakati kile cha mwanzo kipo.

so hapo hakuna mchezo mchafu, cha msingi mtafute mwanasheria wasaidie hata kuiomba benki iwaongezee muda wa kulipa deni, hasa kwa kuomba zuio mahakamani ili hilo gari lisiuzwe.
 
Back
Top Bottom