Wakuu salaam.
Kuna ndugu yangu alikuwa anaumwa malaria kali,ikabidi awekewe catheter kwani alikuwa hajitambui. Baada ya siku mbili alitolewa huo mrija na kuruhusiwa kurudi nyumbani. Lakini wakati wanamtoa,wale manesi walifanya kosa na ikatoka damu nyingi sana,lakini mwisho wa siku wakasema wamerekebisha. Baada ya siku kadhaa akaanza kupata maumivu makali sana na damu kutoka wakati wa kujisaidia haja ndogo. Ameenda hospitali na kufanya vipimo kadhaa vya U.T.I lakini vyote ni negative. Tunaomba msaada wa wataalamu wa njia ya mkojo.