Msaada wa wazo la biashara (Dar es Salaam)

Msaada wa wazo la biashara (Dar es Salaam)

Hot27

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2020
Posts
372
Reaction score
691
Habari za wakati huu nduguzangu. Mungu ni mwema juu ya mapitio yote ya hapa na pale naamini sote tu wazima, penye walakini Mungu alete neema. Nilifanikiwa kupata ID ya mtihani siku ya mtihani (kwa wanaokumbuka, nitaelezea kilichonipelekea hapo kwa wakati mwingine)

Mimi ni kijana wa kiume (22) Nipo Mwanza ila mimi ni mwenyeji wa Dar es salaam, natarajia kumaliza elimu yangu ya chuo kikuu (degree) inshallah inapotimu mwezi wa nane hivyo nitarejea nyumbani Dar es Salaam.

Mungu ni mkubwa nimebahatika kukutana na watu mbalimbali walioweza kunisaidia kwa namna moja ama nyingine. Dhumuni la kuandika uzi huu ni kuwa nahitaji ama naomba kupata wazo la harakati ama biashara yenye mtaji usiozidi laki 6 ambayo naweza kuifanya hasa kwa mkoa wa Dar es salaam (nje na hapo nitaangalia) ili niweze kuanza harakati za maisha.

Nipo tayari kujibu maswali na kuchambua kila ushauri utakaotolewa. Naomba msaada wenu niweze pata mwanga juu ya hilo

Binafsi nimesomea Mass Communication (Mawasiliano ya Umma) ama uandishi wa habari, pia ni muongeaji kiasi (nimewahi kufanya kazi stendi kwenye harakati za kujikimu chuo).

NATANGULIZA SHUKRANI ZANGU ZA DHATI KWENU
 
Dah hongera sana kwakujielewa.laki6 ni ndogo sana napia ni kubwa sana km utapata chanel y biashara.
 
Back
Top Bottom