Msaada wa yeyote anayeweza kunisaidia, unahitajika tafadhali

Msaada wa yeyote anayeweza kunisaidia, unahitajika tafadhali

TheHustler

New Member
Joined
Oct 17, 2024
Posts
3
Reaction score
3
Ni matumaini yangu nyote mko salama.

Ingawa nipo na ID mpya, mimi ni mwanachama wa muda mrefu.

Mimi ni mwanaume, na nimejikuta katika hali ya kulea pacha ambao mama yao aliwaacha wakiwa na mwaka mmoja na nusu. Wakati huo nilikuwa Dar es Salaam kwa shughuli za kutafuta riziki. Niliamua kumtafuta mzazi wa mama yao ili kuzungumza kuhusu mustakabali wa watoto. Kwa bahati mbaya, nilipata jibu la kuwa "kuzaliwa na kulelewa kunatosha" na kwamba kulea wajukuu si jukumu lake.

Nimejaribu hata kutafuta mtu wa kusaidia kuwalea, lakini juhudi hizo hazikuzaa matunda. Kutokana na muda mrefu kutokuwepo kwangu kwenye nyumba niliyopanga, niliamua kurudisha chumba. Baadaye, niliwasiliana na baadhi ya watu, na mmoja wao aliahidi kusaidia baadhi ya mahitaji, hivyo nikaamua kurudi jijini.

Sasa nipo Dar es Salaam, lakini kumpata huyo mtu aliyeniahidi msaada si rahisi, na gharama za malazi kwenye lodge pamoja na matumizi ya watoto ni changamoto kubwa. Nina kazi ya mtandaoni ambayo inaweza kusaidia kidogo, lakini kipato chake hakiwezi kufikia mahitaji yote kama kodi ya nyumba na gharama nyingine kwa wakati mmoja, hasa kwa kuwa nimeanza kazi hiyo muda mfupi uliopita na sijapata nafasi ya kuweka akiba.

Kilichonifanya nirudi jijini ni kwamba nina baadhi ya vitu vyangu vya matumizi na pia fursa za Dar es Salaam ni tofauti na mikoani, ambako maendeleo ni duni. Ombi langu ni kama kuna mtu ana chumba au nyumba iliyowazi, anisaidie japo kwa miezi mitatu ili niweze kubana matumizi na kujipanga kwa ajili ya kodi. Mungu akipenda, hali inaweza kubadilika na mambo kwenda sawa.

Kwa sasa, hali ni ngumu sana. Walezi wenye uzoefu wa kulea watoto wadogo wanaweza kuelewa changamoto hizi. Naomba maombi yenu, lakini pia kama kuna mtu ana uwezo wa kunisaidia hata kwa unga ili watoto wangu waweze kusogeza siku, nitashukuru sana. Nina imani kuwa siku moja nitaweza kuwahudumia kwa uwezo wangu mwenyewe.

Ninatoa shukrani za dhati kwa yeyote atakayesaidia. Pia, kama kuna mtu ana kazi nyingine ya mtandaoni ninayoweza kufanya ili kupata kipato cha ziada, naomba aniambie. Niko tayari kujitahidi ili kuhakikisha ninawalea watoto wangu kwa uangalifu.

Asanteni sana.
 
Back
Top Bottom