LUS0MYA
JF-Expert Member
- Aug 4, 2011
- 866
- 1,109
Ninaye binti yangu mwenye umri wa miaka 13 ambaye anasoma kidato cha kwanza.tatizo la huyu binti ni kushindwa kufanya vizuri katika mitihani yake.Anapofundishwa anaelewa vizuri lakini tatizo ni katika kufanya mitihani.mara nyingine hupata maksi za chini hata zero!ukirudia yale maswali mengi anakuwa anaweza kuyajibu.Utambuzi na uelewa alio nao haufanani na matokeo anayopata katika mitihani yake.Jambo la kushangaza alifaulu kwenda kidato cha kwanza na hata alipofanya mtihani katika shule moja ya kikatoliki alifaulu vizuri na ndio sehemu anaposoma hadi sasa.lakini masista walinipigia simu hivi karibuni na kunijulisha kuwa matokeo yake ya mitihani darasani ni mabaya hivyo wanaweza kumuondoa pale shuleni.Historia ya binti huyu ni kuwa alichelewa sana kuongea na hata uwezo wake wa kujieleza ulichelewa hadi kama darasa la nne.