Msaada wadau kwa binti yangu

LUS0MYA

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2011
Posts
866
Reaction score
1,109
Ninaye binti yangu mwenye umri wa miaka 13 ambaye anasoma kidato cha kwanza.tatizo la huyu binti ni kushindwa kufanya vizuri katika mitihani yake.Anapofundishwa anaelewa vizuri lakini tatizo ni katika kufanya mitihani.mara nyingine hupata maksi za chini hata zero!ukirudia yale maswali mengi anakuwa anaweza kuyajibu.Utambuzi na uelewa alio nao haufanani na matokeo anayopata katika mitihani yake.Jambo la kushangaza alifaulu kwenda kidato cha kwanza na hata alipofanya mtihani katika shule moja ya kikatoliki alifaulu vizuri na ndio sehemu anaposoma hadi sasa.lakini masista walinipigia simu hivi karibuni na kunijulisha kuwa matokeo yake ya mitihani darasani ni mabaya hivyo wanaweza kumuondoa pale shuleni.Historia ya binti huyu ni kuwa alichelewa sana kuongea na hata uwezo wake wa kujieleza ulichelewa hadi kama darasa la nne.
 
anapokuwa kwenye chumba cha mtihan huwa anapanic,yampasa arelax na kufanya mtihan kwan uwoga ni chanzo cha kushndwa kwake mitihan.
 
Nadhani mtoto wako atakua na dyslexia ambayo watu wengi ma genius walikua nayo kama albert einstein Hii..huyo mtoto anahitaji special school ambayo inajumuisha continous assessment na final exams. Hii inasadia sana haswa pale continuos assessment inapo chukua sehemu kubwa ya final exams...mfano CA 70% final exams 30%. Hii nadhani itakua vyema.

vilevile jaribu explore interests za mtoto wako kwa mnunulia toy mbalimbali au kumshirika katika academic shows mbalimbali kama high school science fair projects,essay competitions debate clubs...music dance and drama, art and crafts kama uchoraji na uchongaji nk...hii itakusaidia kugundua ana kipaji gani au ana interest gani.baada ya hapo tafuta mentors wa kumguide huyo mtoto.ili aweze kufanikisha..nadhani mkuu ukifanya haya mtoto atakua one of the great personalities the world will come to know..because the truth is she is a GENIUS....
 

Speech and Psycho Therapy, shile maalumu
 
tafuta wataalam wa mambo ya akili, sidhani hili ni tatizo unaloweza kutatua wewe. Kuna magonjwa aliyotaja mdau mmoja hapo kama dyslexia n.k yanaweza kuwa chanzo.

Unaweza kumuona mtoto bogus kumbe ka-genius fulani.
 
Swalii wewe mwenyewe ulikua na uwezo darasani?

Na vipi wadogo zake kama anao nauwaonavyo wanatofautiana usikute baba mam wote ziroo mmepata helaa maisha sasa mnataka mtoto afauluu akati wazazi wakee wotee maziro?

Akili ya darasani hufuata mkondoo na akili ya maishaa ni juhudii za mtuu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…