Msaada: Wafanyabiashara ya viatu, nguo za ndani Kariakoo

jogijo

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2019
Posts
260
Reaction score
495
Habari ya jumapili wakuu!

Kwa heshima zote naomba msaada nisaidiwe maeneo yanayouza vitu vifuatavyo kwa jumla Kariakoo

I. Viatu simple na slippers
ii. Nguo za ndani, yaani chupi, boxer night dress n.k
iii. Body spray.

Kwa uzoefu wangu, nimefika dar, Mara kadhaa na nikapata simple kwa 5500-5800 kwenye hayo maduka ya wachina. Lakini zile slippers ndio sijui kabisa zinapatikana wapi!

Maduka ya nguo za ndani nalifaham moja lkn nina imani yako mengi na Bei tofauti.

Au Kama kuna mtu aniconnect na supplier wa mikoani! Am humbled.
 
Kituo cha mwendo kasi pale polisi upande wa Ddc pale utapata sliper zote upande ule mwingine utapata sliper na nguo za ndani. Sliper ukinunua kwa box unatoboa.
 
Kituo cha mwendo kasi pale polisi upande wa Ddc pale utapata sliper zote upande ule mwingine utapata sliper na nguo za ndani
Sliper ukinunua kwa box unatoboa
Box shilingi ngap wanauza na zinakua pair ngapi?
 
Nina mtu wa duka la nguo za ndani, Bei zake ni rafiki. Jumla anauza kuanzia 9500 mpaka 42000.
 
Kituo cha mwendo kasi pale polisi upande wa Ddc pale utapata sliper zote upande ule mwingine utapata sliper na nguo za ndani. Sliper ukinunua kwa box unatoboa.
Shukrani lengo langu n box ndugu! Wale wanaopanga pale barabarani Bei zao kubwa kuliko mikoani
 
Ukishuka msimbazi kituo cha kwanza upande wa kulia kuna maduka ya mawigi meengi yanaonekana nje nenda nyuma ya hayo maduka kuna stendi ya zaman ya daladala apo kuna maduka ya vipodozi mwanzo mwisho hata ya chupi unaweza yapata hapo,. Hapo hapo msimbazi upande wa kushoto polisi mbele yake kuna sheli ya total nenda barabara inayo fuata kuingia mtaani kuna maduka yame ambatana na baa ya ddc uko kooote kumejaa slippers/sandals na viatu aina zote ukiwa mitaa hiyo hiyo kwa nda uko fanya kama una ufata mtaa wa kongo kuna maduka ya nguo na boksa huwezi kuzikosa umo nakumbuka walikua wanauza 8k kwa zile boks zenye pc3 ambapo ww utauza kwa 12k
 
Mkuu nahitaji msaada wa kufika katika maduka ya wachina wanao uza nguo kwa bei ya jumla
 
Mimi nauza ndala kutoka China ni nzuri bei chee nauzia online kama unatak njoo pm pia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…