Msaada wakisheria wa Haraka kuinusuru Biashara yangu

Bm_boy

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2013
Posts
547
Reaction score
347
Habari wakuu.
Kama kichwa cha habari kinavyoeleza me ni mjasiria mali mdogo.

Nimepanga chumba ambacho ndicho ninachofanyia biashara yangu. Toka mwaka 2013. Katika kipindi chote nilikua nikimlipa muhusika kodi kwa miezi 3 mi 3. Mwanzo tuliandikishiana mkataba wa miezi 3 ikiws na maana kila baada ya miezi 3 tuta renew mkataba kulingana na malipo.
Iliendelea kwa vipindi viwili nikiwa na maana Tuliandikishana ile miezi 3 ya mwanzo na inayo fuata.. Baada ya hapo ikawa ni kimatendo tuu.. Yani napeleka hela ya miezi mitatu napewa tu risiti ila hatukua tuta renew mkataba kama awali.
Sasa kinachonifanya niombe msaada wakisheria kwa sasa.. Malipo yangu yaliisha Tarehe 5/5/2015 nikaenda kwa mwenye nyumba kwaajili ya malipo. Kwanza akaniambia kodi imepanda kutoka sh 80 elfu mpaka laki moja.. Na akawa anataka nimpe hapo. Mzozo ukaanzia hapo.. Tukashindwa kufikiana mufaka akakataa kupokea na kuniambia kama hauwezi hama au nikupe chumba kingine.. Me nikamwambia sitaki chumba kingine na kama ulikua unataka kupandisha kodi ungenipa taarifa mapema.. Me nikaondoka zangu na hela yangu.. Nikakaa kama baada ya mwezi mmoja akaja na fundi wakanikatia umeme na biashara yangu inategemea umeme kwa 90% toka 6/5/2015 mpaka leo 17/5/2015 sijafanya kazi na wakati huo huo pesa ninazo endeshea biashara ni mkopo.. Kiukweli wananirudisha nyuma sana.. Naombeni msaada nianzie wapi kupata haki yangu.

Ila kwa Taarifa nilizopata kuna mtoto wa mwenye nyumba ndio anataka hiyo room afanye yy biashara.
 
Riziki haizuiwi..tafuta alternative location hama hapo, changamoto hiyo kabiliana nayo. Pole kwa maswahibu.
 
mbona hapo mwanzo umedai kuwa unalipa miezi 3,3ml,hapo sijaelewa?!!!!!!!!
 
itaenda kwa wanasheria utapoteza ela nyingi japo utaipata haki yako. achana nae nenda pengine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…