habari zenu ndugu najua jf kuna watu mbali mbali na pia kuna wale mungu amewajalia kuwa madaktari mbarikiwe kwa kazi mnazo zifanya. mimi tatizo nililo nalo tangu mwezi uliopita usiku ninapo lala sikio hutoa kelele tofauti hiyo hali inanisumbua sana nikaenda hospitali wakanipima na kitochi kwa kuwa niliwaeleza jino la mwisho linaota meno ya ukubwani wakasema sikio halina tatizo hivyo hiyo shida inatokana na mishipa ya meno na masikio huwa ni kitu kimoja nikapewa dawa za maumivu lakini hazinisaidii kitu napata shida sikio lenyewe ni la upande wa kulia hili la kushoto halina tatizo naomba ushauri wako natanguliza shukrani ya ASANTE